76. Thawabu kwa atakayelitamka neno hilo (la Tawhiid) mara kumi


ثواب من قالها عشرا

وعن أبي أيوب رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((من قال لا إله إلا الله وحده لا شريك له ، له الملك وله الحمد ، وهو على كل شيئ قدير ، عشر مرات. كان كمن أعتق أربعة أنفس من ولد إسماعيل)).
[صحيح: رواه البخاري (٢٤٠٤)، ومسلم (٢٦٩٣)]

Na imepokelewa kutoka kwa Abiy Ayyuub (Allaah amridhie) , kwamba hakika Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Yeyote atakayesema hakuna Mola apasayekuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, peke yake hana mshirika, ufalme ni wake , na himidi ni zake, na yeye juu ya kila kitu ni Muweza, mara kumi. Atakuwa sawa (kiujira na malipo) na aliyewaacha huru wanne katika watoto wa (Nabii) Ismail (‘alayhis-salaaam)”.
Sahihi: Ameipokea Bukhary (2404), na Muslim (2693).

Tanbiih:

adhkaari zilizokuja katika shari’ah zisomwe kwa lugha ya kishari’aha.

Muhusika: Shaykh Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.24
Imehaririwa: 27’shab/1438H