81. Thawabu za aina nyingine (za adhkaar) zilizosheheni


ثواب نوع آخر جامع

عن جويرية رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم خرج من عندها بكرة حين صلى الصبح وهي في مسجدها، ثم رجع بعد أن أضحى وهي جالسة، فقال: ((ما زلت على الحال التي فارقتك عليها؟ قالت: نعم، قال النبي صلى الله عليه وسلم : ((لقد قلت بعدك أربع كلمات ثلاث مرات، لو وُزِنَتْ بما قلت منذ اليوم لوزنتهن: سبحان الله وبحمده عدد خلقه، ورضا نفسه، وزنة عرشه، ومداد كلماته)).
[صحيح : رواه مسلم (٢٧٢٦)، والترمذي (٣٥٥٥)]

Imepokelewa kutoka kwa Juwariyyah (Allaah amridhie), kwamba hakika Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) alitoka nyumbani kwake baada ya kuswali subhi akamuacha katika sehemu yake ya kuswali, kisha akarudi Mtume (swalla Llaah ‘alayhi wasallam) akamkuta bado amekaa (katika muswalla wake) , akasema kumwambia:-
“(Bado ungalipo katika hali niliyokuacha nayo?
akasema:-
Ndio.
akasema Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):-
“Hakika baada ya kuondoka kwako nimesema maneno manne tu mara tatu lau yangelinganishwa na yote uliyoyasema (wewe) bila shaka yangelingana:

سُبْحاَنَ اللَّهِ وَبِحَمْدِه
عَدَدَ خَلْقِهِ
وَرِضَا نَفْسِه
وَزِنَةَ عَرْشِهِ
وَمِدَادَ كَلِمَاتِهِ

“Utakasifu wa kutakasika na sifa zenye mapungufu na dosari ni wa Allaah na himdi ni zake.
(Namtakasa) kwa idadi ya viumbe wake.
Na ridhaa za nafsi yake.
Na kwa uzito wa ‘Arshi yake.
Na kwa wingi wa maneno yake”.

Sahihi: Ameipokea Muslim (2726), na Al-Tirmidhiy (3555).

 

Muhusika: Shaykh Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.25
Imehaririwa: 15’ramadhan/1438H