87. Thawabu zilizopo katika adhkaar zinazosomwa baada ya swala za faradhi


 

ثواب أذكار عقب المكتوبات

عن كعب بن عجرة رضي الله عنه، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم. قال: ((معقبات لا يخيب قائلهن- أو فاعلهن -دبر كل صلاة مكتوبة: ثلاث وثلاثون تسبيحة، وثلاث وثلاثون تحميدة، وأربع وثلاثون تكبيرة))

[صحيح: رواه مسلم (٥٩٦)]

Imepokelewa kutoka kwa Ka’ab Ibn ‘Ujrah (Allaah amridhie) , kutoka kwa Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:

“Mu’aqqibaat (maneno ya tasbiih yanayosomwa na kurudiwarudiwa kila baada ya swala) hatoondoka patupu atakayeyasema maneno hayo kila baada ya swala ya faradhi.”

● Tasibihi
(kusema subhaanallaah) mara thelathini na tatu.

● Na tahmiid
(kusema alhamdulillaah) Mara thelathini na tatu.

● Na takbiir
(kusema Allaahu Akbar) mara thelathini na nne”.

Sahihi: Ameipokea Muslim (596).

 

عن أبي هريرة رضي الله عنه – وهذا حديث فتيبة – أن فقراء المهاجرين أتوا رسول الله صلى الله عليه وسلم فقالوا: ذهب أهل الدثور بالدرجات العلى والنعيم المقيم. فقال: ((وما ذاك؟)). قال: يصلون كما نصلي، ويصومون كما نصوم، ويتصدقون ولا نتصدق، ويعتقون ولا نعتق. قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((أفلا أعلمكم شيئا تدركون به من سبقكم، وتسبقون به من بعدكم، ولا يكون أحد أفضل منكم إلا من صنع مثل ما صنعتم؟)). قالوا: بلى يا رسول الله! قال: ((تسبحون الله وتكبرون وتحمدون دبر كل صلاة ثلاثا وثلاثين مرة)). قال أبو صالح: فرجع فقراء المهاجرين إلى رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فقالوا: سمع أخواننا أهل الأموال بما فعلنا، ففعلوا مثله. فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((ذلك فضل الله يؤتيه من يشاء)). قال سمي: فحدثت بعض أهلي بهذا الحديث فقال: وهمت إنما قال: ((تسبح الله ثلاثا وثلاثين، وتحمد الله ثلاثا وثلاثين، وتكبر الله ثلاثا وثلاثين)). فرجعت إلى أبي صالح فقلت له ذلك فأخذ بيدي ، وقال: ((تقول: الله أكبر وسبحان الله والحمد لله حتى تبلغ من جميعهن ثلاثا وثلاثين))

[صحيح: رواه البخاري (٦٣٢٩) ، ومسلم (٥٩٥)]

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie), -na hii ni riwaya kutoka kwa Qutaybah- :

“Kwamba mafukara wa kimuhaajiriina walimjia Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) wakasema:

“Wamejiondokea (wenzetu) wenye mali (nyingi) kwa daraja za juu kabisa (peponi) na starehe za kudumu.”

Akasema Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):

“haya kulikoni?”.

Wakasema:

(Wenzetu) wanaswali kama tunavyoswali, wanafunga kama tunavyofunga, na wanatoa sadaka na sisi hatutoi sadaka, wanawaacha watumwa huru na sisi hatuna uwezo huo.

Akasema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):

“Hivi nisikufunzeni jambo mkilifanya mtawadiriki waliokutangulieni, na mtawapita watakaokuwa nyuma yenu!?
Na wala hatopatikana yeyote atakayekuzidini kwa ubora zaidi ya yule atakayefanya mithili ya mfanyavyo!?

Wakasema:

Tujuze ewe Mtume wa Allaah!

Akasema:

“Msabihini Allaah (subhaanallaah), na mtukuzeni (Allaahu Akbar), na mhimidini (alhamdulillaah), kila baada ya swala mara thelathini na tatu”.

Anasema Abuu Swaalih (mpokezi wa hadithi hii kutoka kwa Abuu Hurayrah):

Wakarudi tena Hawa mafukara wa kimuhaajiriina kwa Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) wakamwambia:

“Wameyasikia yale mafunzo (uliyotufunza) ndugu zetu wenye mali na wao wanayasema pia”.

Akasema Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):

” Hizo sasa ni fadhila za Allaah humpa amtakaye”.

Anasema Sumayyun (mmoja katika wapokezi wa hii hadithi kutoka kwa Abuu Swaalih):

“Nikamuhadithia mmoja wa watu wangu hadithi hii, akaniambia:

“Umekosea! (Yaani katika namna ya mpangilio wa hizo tasbiih), hakika yeye amesema:

” Msabihi Allaah mara thelathini na tatu, mhimidi Allaah mara thelathini na tatu, mtukuze Allaah mara thelathini na tatu”.

Anasema Sumayyun:

“Nikarudi tena kwa Abuu Swaalih, nikamweleza hayo (niliyoambiwa), akaukamata mkono wangu na kusema:

” Sema Allaahu Akbar, na Subhaanallaah, na Alhamdulillaah mpaka zote hizo zitimie Mara thelathini na tatu”.

Sahihi: Ameipokea Bukhariy (6329) , na Muslim (595).

Tanbiih 1:

Imekuja katika mapokezi mengine kutoka katika hadithi ya Abuu Dharr (Allaah Amridhie) kuwa Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) aliwaambia:

“Kwani si tayari Allaah ameshakujaalieni Yale ambayo mkiyafanya mtakuwa sawa na wanaotoa sadaka!

Hakika kila tasbiih ni sadaka, na kila takbiir ni sadaka, na kila tahmiid ni sadaka, na kila tahliil ni sadaka, kuamrisha mema ni sadaka, kukataza maovu ni sadaka, na kwenye tupu ya mmoja wenu pia kuna sadaka (yaani katika tendo la ndoa)”Al-Hadiith.

Tanbiih 2:

Maneno waliyoyasema Mafukara wa kimuhaajiriina hayanuki harufu ya hasada si kwa mbali wala kwa karibu, na wametakaswa Maswahaba wa Mtume wetu (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) kutokana na jambo hilo na mengineyo. Bali huo ni wivu wa kimaendeleo (إن صح التعبير) ambao huitwa kwa lugha ya shari’a “ghibtwah”, na ni katika mambo ambayo Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) ameyaruhusu akasema:

“Hakuna hasadi inayofaa isipokuwa katika mambo mawili

1. Mtu aliyepewa na Allaah mali akawa anaitumia katika wujuhu (nyanja) za kheri.*
2. Na mtu aliyepewa na Allaah Elimu (ya Dini) akawa anaitumia na kuwasaidia wenzake”.

Na hasadi iliyokusudiwa hapa ni wewe utamani uwe kama hao watu wawili pasi na kutamani Neema aliyepewa mwenzako imuondoke.

Tanbiih 3:

Dhahiri ya njia zilizopokelewa katika kuonesha namna ya hizi tasbiih baada ya swala ni kwamba anatakiwa Muislam aseme “subhaanaLlaah” mara thelathini na tatu, na “Alhamdulillaah” mara thelathini na tatu, na “Allaahu Akbar” mara thelathini na tatu, na njia hii ni awlaa kuliko tafsiri ya Abuu Swaalih. Na haya ameyasema Al-Qaadhiy ‘Iyaadh (Allaah amrehem) , ameyanukuu haya Al-Imam Al-Nawawiy.

Muhusika: Shaykh Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjim: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy Uk.27-28
Imehaririwa: 29’Rthaaniy/1439H