90. Thawabu kwa atakayeshukia mashukio yoyote akayasoma maneno haya


 

ثواب من نزل منزلا فقال هذه الكلمات

عن خولة بنت حكيم السلمية قالت: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: (( من نزل منزلا ، ثم قال: أعوذ بكلمات الله التامات من شر ما خلق لم يضره شيئ حتى يرتحل من منزله ذلك))

[صحيح: رواه مسلم (٢٧٠٨)]

Imepokelewa kutoka kwa Khawlah bint Hakiim Al-Sulamiyyah (Allaah amridhie) amesema:

Nilimsikia Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) akisema:
“Yeyote atakayeshukia popote (iwe mjini,kijijini shambani na kwengineko), kisha akasema:
Najikinga kwa maneno ya Allaah yaliyotimia , kutokana na shari ya alivyoviumba.
→ Hatodhuriwa huyo na chochote mpaka atakapoondoka kutoka katika mashukio yake hayo”.

Sahihi: Ameipokea Muslim (2708).

º● Faida:●º

Amesema Al-Imam Al-Qurtubiy (Allaah Amraham):

“Na hii ni khabari sahihi kabisa, na ni kauli ya kweli, tumeujua ukweli wake kwa dalili na majaribio, kwani mimi (Al-Qurtubiy) tangu nilivyoisikia hadithi hii nilikuwa nikiifanyia kazi , sikuwahi kudhuriwa na chochote mpaka siku nilipoacha (kuisoma) niliumwa na Nge mahdiyah (jina la mji) usiku, nikatafakari nafsini mwangu nikakumbuka kuwa nilisahau kuomba kinga kwa haya maneno”.

Rej: “Fat’hul-Majiid” (177-178) Daarul-Ghadi.

Muhusika: Shaykh Ikhtiyaar ‘Ubayd
Kiunganishi: http://duaatsalaftz.net/category/makala/miirathun-nabiyy/
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: miiraathun-Nabiyy Uk.28-29
Imehaririwa: 1’J-Uwlaa/1439