94. Thawabu kwa atakayemuombea nduguye kwa hali ya siri


 

◆ ثواب من دعا لأخيه بظهر الغيب◆

عن أبي الدرداء رضي الله عنه ، أنه سمع رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((ما من عبد مسلم يدعو لأخيه بظهر الغيب إلا قال الملك: ولك بمثل))

وفي رواية: أن النبي صلى الله عليه وسلم كان يقول: ((دعوة المرء المسلم لأخيه بظهر الغيب مستجابة، عند رأسه ملك موكل كلما دعا لأخيه بخير، قال الملك الموكل به: آمين ، ولك بمثل))

[صحيح: رواه مسلم (٢٧٣٢)]
Imepokelewa kutoka kwa Abud-Dardaa (Allaah amridhie) , kwamba hakika yeye alimsikia Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) akisema:
“Hakuna mja yeyote Muislam atakayemuombea nduguye (dua njema) kwa siri isipokuwa atasema Malaika:
“Na wewe upate mfanoe”.
Na imekuja katika mapokezi mengine, kwamba Hakika Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) alikuwa akisema:
” Dua ya mtu Muislam kwa nduguye iyombwayo kwa siri ni yenye kukubaliwa. Kichwani mwake (muombaji) kuna Malaika aliyewakilishwa (na Allaa), kila pale ambapo anamuombea nduguye ya kheri, husema Malaika aliyewakilishwa:
“Aamiin!”.
Na wewe upate mfano wake”.
Sahihi: Ameipokea Muslim (2732).

■ Faida: ■

Amesema Al-Imam Al-Nawawiy (Allaah amraham):-

” وكان بعض السلف إذا أراد أن يدعو لنفسه يدعو لأخيه المسلم بتلك الدعوة، لأنها تستجاب، ويحصل لها مثلها “. المنهاج

“Alikuwa mmoja katika Wema waliotangulia (Salaf) anapotaka kujiombea dua ,huwa anamuombea nduguye Muislam kwa dua yake hiyo, kwa sababu hukubaliwa na yeye akapata mfano wake”

● Faida:●

Na amesema Al-‘Uthaymiin (Allaah amraham):-

“(Dua kama hii) hujulisha kwa uwazi kabisa juu ya ukweli wa imani (ya Mtu), kwa sababu Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:_

”لا يؤمن أحدكم حتى يحب لأخيه ما يحب لنفسه”

“Hatokuwa mmoja wenu ni muumini mkamilifu wa Imani mpaka ampendelee nduguye kile akipendacho nafsini mwake”.
Kwahiyo utakapomuombea nduguye kwa siri (mbali na hadhra yake) bila ya yeye kukuusia wewe kwa hilo. Bila shaka hilo huwa ni dalili juu ya mapenzi yako kwake yeye” (Sharh Riyaadh).

Muhusika: Shaykh Ikhtiyaar ‘Ubayd
Kiunganishi: http://duaatsalaftz.net/category/makala/miirathun-nabiyy/
Mtarjim:http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: miiraathun-Nabiyy Uk.30-31
Imehaririwa: 8’J-Uwlaa/1439H