95. Thawabu kwa atakayemuomba Allaah pepo na akamuomba amkinge kutokana na moto


 

■ ثواب من سأل الله الجنة واستعاذ من النار■

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((ما استجار عبد من النار سبع مرات ، إلا قالت النار: يا رب إن عبدك فلانا استجار مني فأجره، ولا سأل عبد الجنة سبع مرات ، إلا قالت الجنة: يا رب! إن عبدك فلانا سألني فأدخله الجنة))

[صحيح: رواه أبو يعلى (٦١٩٢) ، والحاكم ، وقال: صحيح الإسناد ، وصححه الألباني في “صحيح الترغيب” (٣٦٥٣)]
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie) , amesema:
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Hakuna mja yeyote atakayeomba (kwa Allaah) akingwe kutokana na moto Mara saba , ila moto huwa ukisema:
Ewe Mola wangu! Hakika mja wako Fulani ameomba kukingwa nami, hivyo mkinge.
Na wala hakuna mja yeyote atakayeomba pepo mara saba , ila itasema Pepo:
Ewe Mola wangu! Hakika mja wako Fulani ameniomba Mimi basi muingize Peponi”.
Sahihi: Ameipokea Abuu Ya’alaa (6192) , na Al-Haakim , na akasema: Isnad yake ni sahihi. Na Ameisahihisha Al-Albaaniy (Allaah amraham), katika “Sahiihut-Targhiib” (3653).

◆ Faida:◆

Amesema Al-Albaaniy (Allaah Amraham):

“Hakika wamezoea baadhi ya watu katika mji wa Damascus na Miji mingineyo ,kuisoma hii dua iliyotajwa kwa idadi ya saba katika hadithi hii, tena (huisoma) kwa sauti ya juu na kwa pamoja Mara tu baada ya swala ya alfajiri. Na jambo hili ni miongoni mwa Yale ambayo sijayajulia kuwa yana asili katika sunnah takasifu. Na wala haifai kuitegemea hadithi hii (yaani kuijengea hoja kwa kusoma kwao kwa sauti na kwa pamoja) , kwani hadithi hii imeenea (kwa wakati wowote) haikudhibitiwa kwa swala ya alfajiri (tuu) wala swala ya jamaa….. Kwahiyo atakayetaka kuifanyia kazi hadithi hii basi ayaseme maneno hayo wakati wowote iwe usiku au mchana , kabla ya swala au baada yake”. (Al-Sahiiha 6/22).

Hivyo utasema:

 

أللهم أجرني من النار ×7
اللهم إني أسألك الجنة ×7

Na mfano wa maneno kama hayo.

والله أعلم.

Muhusika: Shaykh Ikhtiyaar ‘Ubayd
Kiunganishi: http://duaatsalaftz.net/category/makala/miirathun-nabiyy/
Mtarjim:http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: miiraathun-Nabiyy Uk.31
Imehaririwa: 8’J-Uwlaa/1439H