ADABU ZA KUULIZA SWALI KWA WANAZUONI NA MASHEIKH!!


المقدمة
UTANGULIZI
الحمد لله ، نحمده ، ونستعينه، ونستغفره، ونعوذ بالله من شرور أنفسنا ومن سيآت أعمالنا، من يهدي الله فلا مضل له ومن يضلل فلا هادي له
وأشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له، وأشهد أن محمدا عبده ورسوله
Huu ni mwanzo mzuri wa makala zitakazohusu ubainifu juu ya adabu za kuuliza ambazo anapaswa kuzijua mwanafunzi katika Ahlus-Sunnah mbele ya walimu zake .
Na asili ya hizi makala ambazo inshaa Allaah tutakuwa tunazitoa kidogo kidogo kulingana wa tawfiiq ya Allaah katika muda na wasaa na ufanisi, ni muhadhara wa kielimu ambao aliutoa fadhiilat Al-Shaykh Swaalih Aalish- Shaykh -Allaah amhifadhi!- Alioupa anuani:
أدب السؤال
Yaani: adabu za uulizaji swali.
Na yale yote ambayo yatampasa kuyajua kila muulizaji katika maswali yake, na muulizwa katika majibu yake.
Na yanayopasa kuchungwa juu ya hilo, ili kujaalia faida iwe ni yenye kupatikana, na fitina kuepukana.
fitina ambayo huenda ingepatikana kwasababu ya maswali ambayo nwenye maswali hayo ameshindwa kuyaweka katika nuundo mzuri, na akayauliza mbele ya hadhira ya watu ambao ni wakawaida wasiojishughulisha na elimu, ambao kwa lugha ya kitaalamu huitwa {العوام}.
Tunamuomba Allaah atupe tawfiiq katika kuliendea hili, na aturuzuku iklhasi katika amali zetu , na atupe husnal-khaatimah, na atuthibitishe katika haki na uongofu na sunnah , mpaka tufike kwake katika ile siku tuliyoahidiwa.
إنه ولي ذلك والقادر عليه، وصلى الله وسلم على نبينا محمد وآله وصحبه وسلم
Muhusika: duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 10’jumaadal-uwlaa/1438H