‘Aqiqa Ya Kisheria


Swali:
assalam alaykum warahmatullah wabarakaatuh
je ni ipi hakik ya kisuna inavyotakiwa kufanyika? na yapi ya kuepuka?
baarakallahu fiykum
Jawabu:
Aqiqa ni mnyama wa sadaka anaechinjwa siku ya saba tangu analipozaliwa mtoto.
Mnyama huyo ni mbuzi wawili kwa mtoto wa kime na mbuzi mmoja kwa mtoto wa kike.
Baada kuchinjwa nyama itagawiwa maskini ikiwa imepikwa ni bora zaidi.
Si vibaya kuwaita nyumbani ndugu jamaa na marafiki kushiriki kula aqiqa.
Mtoto atapewa Jina siku hiyo na atanyolewa kwa mara ya kwanza.
Nywele zitatupwa kama nywele nyingine.
Mifupa ngozi ya aqiqà hazina tofauti na nyama nyingine ktk kuivunja na kuitafuna.
Kama umepitwa kufanya aqiqa siku ya saba basi utafanya siku ya 14 au 21.
Na kama ulikua hujui jambo hili ukajalijua muda umeshapita basi waweza kulifanya muda wowote lakini lina tofauti za ulamaa.
Kuna mambo yanaongezwa ktk aqiqa hayapo kama vile kula nyama hiyo na asali, kutovunja mifupa,kuikusanya mifupa yote pamoja na ngozi na kuizika pamoja, Hakuna usahihi wowte ktk hayo.
Masharti ya mnyama atakaechinjwa ni yaleyale ya mnyama wa Udh hiya. Asiwe kilema chongo aliekonda sana mwenye kasoro mbaya (aibu) nk Wallahu a’alam
Muhusika: duaatsalaftz
Chanzo: www.duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 12/10/2016