05. Thawabu kwa atakayeswali swala ya isha na as-subhi katika jamaa’ah


Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie) amesema,
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Swala nzito juu ya wanafiki ni swala ya isha na swala ya al-fajiri.
Na lau wangelijua yaliyomo humo wangeziendea (swala hizo) japo kwa kusota (na kutambaa).
Na kwa hakika nimepupia kuamrisha swala ikimiwe, kisha nimuamrishe mtu awaswalishe watu, kisha niondoke na kikundi cha watu wakiwa wamebeba vijinga vya moto kuwaendea watu wasiohudhuria swala nizichome juu yao nyumba zao kwa moto”.
Mhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd.
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.4
Imehaririwa: 3’jumaadal-uwlaa/1438H