06. Thawabu za kuitika ‘aamiin’ na yule ambaye kuitika kwake ‘aamiin’ kumeafikiana na kuita kw?a malaika ‘aamiin’


Imepokelewa kutoka kwa mama ‘Aaishah (Allaah amridhie), kwamba hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam), walitajwa mbele yake mayahudi , akasema:
“Hakika wao hawatufanyii uhasidi juu ya kitu chochote zaidi ya wanavyotuhusudu juu ya siku ya ijumaa ambayo Allaah ametuongoza kwayo , na wao wakaipoteza. Na kibla ambacho Allaah ametuongoza kwacho , na kusema kwetu ‘aamiin’ nyuma ya imam”.
ameipokea Ahmad , ibn Maajah na ibn Khuzaymah kwa mukhtasar, na akasema:
“Hakuna kubwa wanalokuhusuduni mayahudi kama ile husda yao juu yenu kwa kuitika ‘aamiin na salamu (yenu)”
Amepokea ibn Maajah (856), ibn Khuzaymah (3/38), Ahmad (6/135), na ameitaja Al-Haythamiyy katika [al-maj’ma’i] 2/15.
Muhusika: Ikthiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.4
Imehaririwa: 3’jumaadal-uwlaa/1438H