08. Thawabu kwa atakayeunga safu au kuziba mwanya wa safu


Imepokelewa kutoka kwa Al-Baraa bin ‘Aazib (Allaah amridhie), amesema:
“Alikuwa Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam), akiikaguwa safu kutoka nchani mpaka nchani, alikuwa akitupanga kwa kutushika mabega yetu na vifua vyetu akisema:
“Msikhtalifiane zitakhtalifiana nyoyo zenu”.
Anasema Baraa, na alikuwa akisema:
“Hakika Allaah na Malaika wake wanawaswalia wale ambao wanaunga safu”.
Ameipokea Ahmad na ibn Maajah. Na amezidisha
“Na yeyote atakayeziba mwanya (wa safu), Allaah atamuinua kwa hilo daraja.
Na wala hakuna hatua yoyote ipendezayo kwa Allaah kama ile hatua atakayoiinua (mtu) kwa lengo la kuunga safu”.
Ameipokea Ahmad (4/285), Abuu Daud (644), ibn Khuzaymah (3/26) na ameifanyia takhriij Al-Albaaniy katika “al-sahiiha” (7256).
Na imepokelewa kutoka kwa Abdullaah bin ‘Umar (Allaah awaridhie)
, kwamba hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Yeyote atakayeiunga safu basi naye ataungwa na Allaah, na atakayeikata safu atakatwa na Allaah”.
Ameipokea Al-Nasaaiy, ibn Khuzaymah, Al-Haakim na akasema:
“sahihi kwa sharti za Imam Muslim”.
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.5
Imehaririwa: 3’jumaadal-uwlaa/1438H