11. Thawabu za kwenda msikitini kwaajili ya swala


Amesema Allaah Mtukufu:
“Enyi mlioamini! Pindi inadiwapo kwaajili ya swala kwa siku ya ijumaa basi harakeni kwenda kwenye utajo wa Allaah na acheni kuuza na kununua, mkifanya hivyo ni bora zaidi kwenu kama mnajua”. [Al-jumuah9].
Na imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie) amesema,
Amesema Mtume wa Allaah (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Yeyote atakayechukua na akaushika vyema udhu wake, kisha akatoka kwa lengo la kuiendea swala, hakika yake mtu huyo atahesabika yupo katika swala muda wakuwa anaidhamiria swala.
Na hakika ataandikiwa kwa moja za hatua zake jema moja, na atafutiwa kwa hatua nyengine kosa moja.
Hivyo asikiapo mmoja wenu iqamah asikimbie.
kwani atakayekuwa mwingi wenu wa ujira (mbele ya Allaah) ni mwenye nyumba iliyo mbali.
Wakasema kumuuliza Abuu Hurayrah:
Kwanini ewe Abuu Hurayrah!?
Akasema:
“Kwasababu ya wingi wa hatua”.
Sahihi: ameipokea Bukhary (647) , na Muslim (649), na Maalik (1/33).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.5-6
Imehaririwa: 3’jumaadal-uwlaa/1438H