14. Thawabu kwa mwenyekuketi msikitini akisubiri swala


Amesema Allaah Mtukufu:
“Enyi ambao mmeamini! Kuweni na subra (juu ya dini yenu), na subirini (juu ya maadui zenu), na zisubirini swala baada ya swala, na muogopeni Allaah ili mupate ufaulu”. [al-imran 200].
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie) , kwamba hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Hatoachakuwa mmoja wenu anahesabika yupo katika swala muda wa kuwa swala ndiyo inayomzuia (yaani anaisubiria).
Na malaika (wanamuombea) wakisema:
“Ewe Allaah! Muhurumie muda wa kuwa hajainuka kutoka sehemu aliyoswalia au kupatwa na hadathi”.
Na katika riwaya ya Muslim:
“Hatoachakuwa mja yupo katika swala muda wa kuwa amebaki pale aliposwali akisubiri swala nyengine”.
Na malaika wanasema:
“Ewe Allaah! Msamehe! Ewe Allaah! Muhurumie! mpaka amalize (kuswali), au apatwe na hadhathi.
Akaulizwa Abuu Hurayrah:
Nini maana ya kupatwa na hadathi!?
Akajibu:
“Afuse au ashute!”.
Sahihi: ameipokea Bukhary (647), na Muslim (649).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.6
Imehaririwa: 4’jumaadal-uwlaa/1438H