22. Thawabu kwa mwenyekulala akiwa twahara


Imepokelewa kutoka kwa Mu’aadh bin Jabal (Allaah amridhie), kutoka kwa Nabiy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam), amesema:
“Hakuna muislam yeyote atakayelala akiwa na twahara kisha akasimama usiku akimuomba Allaah katika kheri za dunia na akhera, isipokuwa Allaah atampa”.
Sahihi: ameipokea Abuu Daud (2401), na Al-Nasaaiy katika “amal-alyawm” (806), na ameifanyia takhriij Al-Albaaniy katika “sahiiha” (3288).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.8
Imehaririwa: 6’jumaadal-uwlaa/1438H