28. Thawabu kwa atakayeuawa kwa kuitetea mali yake,damu,dini mke/jamaa


Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdillaah bin ‘Amri (Allaah awaridhie), amesema:
Nimemsikia Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) akisema:
“Yeyote atakayeuawa kwa kutetea mali yake basi huyo (amekufa) shahidi”.
Na kwenye riwaya ya Al-Tirmidhiy :
Nimemsikia Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) akisema:
“Yeyote ambaye itatakiwa mali yake bila ya haki, akapambana mpaka kuuawa basi yeye ni shahidi”.
Sahihi: ameipokea Bukhary (1251), na Muslim (2632).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.10
Imehaririwa: 9’jumaadal-uwlaa/1438H