32. Thawabu za kulisha chakula liwajhillaah


Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdillaah bin ‘Amri (Allaah awaridhie) , kwamba hakika Mtu mmoja alimuuliza Nabiy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) :
Ni kipi katika mambo ya Uislam bora zaidi!?
Akasema (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Lisha chakula (kwa sadaka au kwa dhifa nk.), na umsalimie umjuae na usiyemjua (katika Waislam)”.
Sahihi: ameipokea Bukhary (12), na Muslim (39).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.11
Imehaririwa: 11’jumaadal-uwlaa/1438H