40. Thawabu katika kula daku


1. Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Allaah amridhie) amesema:
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Kuleni daku (yaani: katika wakati wa theluthi ya mwisho ya usiku), kwani hakika katika kula daku kuna baraka”.
Sahihi: ameipokea Bukhary (1923), na Muslim (1095).
2. Imepokelewa kutoka kwa ‘Irbaadh bin Saariyah (Allaah amridhie) amesema:
Aliniita Mtume wa Allaah (swalla Llaah ‘alayhi wasallam) kwenye kula dawa mwezi wa ramadhani, akasema:
“Njoo kunako chakula chenye baraka”.
Ameipokea Abuu Daud (2344), na Al-Nasaaiy (4/145), na ibn Khuzaymah (1938), na ibn Hibban (3456), na ameisahihisha Al-Albaabiy katika “al-mishkaat” (1997).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.13
Imehaririwa: 14’jumaadal-uwlaa/1438H