41. Thawabu za kuwahi kufuturu


1. Imepokelewa kutoka kwa Sahli bin Sa’ad (Allaah amridhie) ‘ amesema:
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Umma wangu hautoachakuwa umeshikamana na sunna zangu muda wa kuwa hawasubiri nyota wakati wa kufuturu kwao”.
Sahihi: ameipokea ibn Hibban (3501), na ameisahihisha Al-Albaaniy katika “sahiih al-targhiib” (1074).
2. Imepokelewa kutoka kwa Sahli bin Sa’ad (Allaah amridhie) , kwamba hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Watu hawatoachakuwa wapo kwenye kheri muda wa kuwa wanawahi kufuturu”.
Sahihi: ameipokea Bukhary (1957), na Muslim (1098).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.13
Imehaririwa: 14’jumaadal-uwlaa/1438H