43. Thawabu kwa mwenyekufunga siku ya ‘arafah


1. Imepokelewa kutoka kwa Abuu Qataadah Al-Answaariy (Allaah amridhie) , kwamba hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) aliulizwa kuhusu funga ya siku ya ‘arafah, akasema:
“Hufuta madhambi ya mwaka uliopita na uliobaki”.
Sahihi: ameipokea Muslim (1162), na Al-Tirmidhiy (749).
2. Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie), amesema:
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Bora ya funga baada ya funga ya ramadhani ni funga katika mwezi wa Allaah wa muharram, na bora ya swala baada ya swala za faradhi ni swala za usiku”.
Sahihi: ameipokea Muslim (1163).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.13
Imehaririwa: 14’jumaadal-uwlaa/1438H