44. Thawabu kwa atakayefunga siku ya ‘aashuuraa


1. Imepokelewa kutoka kwa Abuu Qataadah Al-Answary (Allaah amridhie) , kwamba hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) aliulizwa kuhusu funga ya siku ya ‘aashuuraa (10/muharram), akasema:
“Hufuta madhambi ya mwaka uliopita”.
Sahihi: ameipokea Muslim (1162).
2. Na kutoka kwake (Allaah amridhie) amesema:
“Hakuna nilijualo kwamba Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) alikuwa akiifunga siku kwa kutaka fadhila zake zaidi ya siku hii (yaani: ‘aashuuraa), na wala hakuna mwezi ila mwezi huu -yaani: ramadhani-“.
Sahihi: ameipokea Muslim (1132).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.14
Imehaririwa: 14’jumaadal-uwlaa/1438H