45. Thawabu kwa atakayefunga siku tatu kila nwezi


1. Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdillaah bin ‘Amr bin Al-‘Aas (Allaah awaridhie) amesema:
Hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Kufunga siku tatu ni sawa na kufunga mwaka mzima”.
Sahihi: ameipokea Bukhary (1979), na Muslim (1159).
2. Na imepokelewa kutoka kwa Qurrah bin Iyaas (Allaah amridhie) , kwamba hakika Nabiy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Kufunga siku tatu kila mwezi ni sawa na kufunga mwaka mzima na kufturu kwake”.
Sahihi: ameipokea Ahmad (3/436), na Al-Bazzar (1059), na ibn Maajah (3652), na ameitaja Al-Haythamiy katika “al-maj’ma’i” (3/196), na ameisahihisha Al-Albaaniy katika “sahiih al-targhiib” (1031).
3. Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharr (Allaah amridhie) , kwamba hakika Nabiy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Yeyote atakayefunga katika mwezi siku tatu hiyo ndio funga ya mwaka”
Allaah-‘azza wajalla- akateremsha usadikisho wa hilo katika kitabu chake akasema:
(من جاء بالحسنة فله عشر أمثالها (الأنعام: ١٦٠
“Yeyote atakayekuja na jema moja basi atapata mara kumi yake”.
Na siku moja ni kwa siku kumi”.
Sahihi: ameipokea Ahmad (5/145), na Al-Tirmidhiy (762), na Al-Nasaaiy (4/219), na ibn Maajah (1708), na ibn Khuzaymah (2126), na ameifanyia takhriij Al-Albaaniy katika “sahiih al-nasaaiy” (2269).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaft.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.14
Imehaririwa: 22’jumaadal-uwlaa/1438H