47. Thawabu za kwenda hija


Amesema Allaah aliyetukuka:
(وَلِلَّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا (آل عمران: 97
“Na Allaah amefaradhisha juu ya watu kwenda kuhiji katika nyumba (yake) kwa mwenyeuwezo wa kwenda huko”.
Na akasema Allaah Mtukufu:
وَإِذْ جَعَلْنَا الْبَيْتَ مَثَابَةً لِّلنَّاسِ وَأَمْنًا وَاتَّخِذُوا مِن مَّقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى ۖ وَعَهِدْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْعَاكِفِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُود (125:البقرة)
“Na(kumbukeni khabari hii pia)Tulipoifanya Nyumba(ya Al-Kaa’ba) iwe mahali pakuendewa na watu na mahali pa salama.Na mahali alipokuwa akisimama Ibrahimu na Ismaili(Tukawaambia):” Itakaseni (isafisheni) Nyumbani yangu kwa ajili ya wale wanao izunguka kwa ajili ya kutufu na wanaokaa hapo na (kwa ajili ya) wanao rukuu na kudujudu hapo pia.”
1. Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie) , kwamba hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
مَنْ حَجَّ فَلَمْ يَرْفُثْ وَلَمْ يَفْسُقْ خرج من ذنوبه كَيَوْمِ وَلَدَتْهُ أُمّه
“Yeyote atakayehiji kisha asizungumze mabaya wala kutenda mabaya, atayatoka madhambi yake awe sawa na siku aliyozaliwa na mama yake”.
Sahihi: ameipokea Bukhary (26), na Muslim (83).
2. Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie), aliulizwa Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
Ni amali ipi (katika Uislam) ni bora zaidi?
Akasema:
“Kumuamini Allaah na Mtume wake”.
Ikaulizwa:
Kisha nini?
Akasema:
“Kuipigania (jihadi) njia ya Allaah”.
Ikaulizwa:
Kisha nini?
Akasema:
“Hija iliyotakaswa”.
Sahihi: ameipokea Bukhary (1521), na Muslim (1350).
3. Na kutoka kwake (Abuu Hurayrah) ,kwamba hakika Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
العمرة إلى العمرة كفارة لما بينهما ، والحج المبرور ليس له جزاء إلا الجنة
” ‘Umrah mpaka ‘Umrah ni kifutio cha madhambi yaliyotendwa baina yake (baina ya umrah mbili hizo), na hija iliyotakaswa (kutokana na madhambi) haina malipo mengine zaidi ya pepo”.
Sahihi: ameipokea Bukhary (1773), na Muslim (1349).
4. Na imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uud (Allaah amridhie) ,amesema:
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Fuatisheni baina ya hija na ‘umrah, kwani hakika viwili hivyo vinaondoa ufakiri na kufura madhambi kama ambavyo moto (wa mfua vyuma) unavyokisafisha chuma na dhahabu na fedha. Na wala hija iliyotakaswa haina malipo mengine zaidi ya pepo”.
Sahihi: ameipokea Al-Tirmidhiy (810), na ibn Khuzaymah (2512), na Al-Nasaaiy (4/219), na ibn Hibban (3685), na ameisahihisha Al-Albaaniy katika “sahiih al-targhiib” (1103).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.15
Imehaririwa: 22’jumaadal-uwlaa/1438H