03. Katazo la kukithirisha maswali


Na asili ya jambo hili la kukithirisha maswali ambalo yamekuja makemeo juu yake.
Imethibiti hadithi katika sahihi mbili kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie), kwamba Nabiy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
ما نهيتكم عنه فاجتنبوه، وما أمرتكم به فأتوا ما استطعتم، فإنما أهلك الذين من قبلكم كثرة مسائلهم واختلافهم على أنبيائهم
“Yale yote niliyokukatazeni basi jiepusheni nayo, na yale niliyokuamrisheni yaendeeni kadiri ya uwezo wenu, kwani hakika kilichowaangamiza waliotangulia kabla yenu ni wingi wa maswali yao, na kwenda kinyume na Manabii wao”.
Wamesema Wanazuoni:
قوله: ((كثرة مسائلهم)) يعني: عما لم يأت بيانه في الكتاب المنزل
Kauli yake Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) aliposema:
“wingi wa maswali yao..”
Anakusudia, yale mambo ambayo hayajatokea , na yale ambayo hayajajiliwa na ubainifu wake kwenye kitabu kilichoteremshwa.
Na ndio maana imekuja katika “sahihi”, kwamba Nabiy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
إن أشد المسلمين جرما من سأل عن شيئ لم يحرم على المسلمين فحرم عليهم لأجل مسألته
“Hakika mwenye ubaya zaidi kwa Waislam, ni yule aliyeuliza kuhusiana na jambo (fulani) ambalo halikuharamishwa, kisha likaharamishwa kwasababu ya kuuliza kwake”.
Na kwa hakika amesema Allaah aliyetukuka:
لا تسألوا عن أشياء إن تبد لكم تسؤكم وإن تسألوا عنها حين ينزل القرآن تبد لكم عفا الله عنها
(المائدة: ١٠١)
“Msiulizie baadhi ya mambo (ambayo hamna haja nayo mpaka mkayauliza, na wala si mambo yanayokuhusuni kwenye dini yenu) mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyauliza inapoteremshwa Qur’aan mtabainishiwa. Allaah ameshasamehe hayo”.
Na hadithi zilizokuja kukemea juu ya kuulizauliza sana ni nyingi.
Muhusika: Shaykh Swaalih Aalish-Shaykh
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: adabus-suaal uk.9
Imehaririwa: 11’jumaadal-uwlaa/1438H