05. Na Allaah-jalla wa’alaa- amewaamrisha Waumini waulize pale


Na kwa hakika amesema Mwenye utakasifu na utukufu, pale walipopinga makafiri wa kiqurayshi kuwa iweje Mtume awe ni mtu!?
Na wakasema hakika ni wajibu Mtume awe ni malaika.
Akasema (subhaanahu wata’aalaa), katika suurat al-nahli:43-44
وَمَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِىٓ إِلَيْهِمْ ۚ فَسْـَٔلُوٓا۟ أَهْلَ ٱلذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ
Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi (Ufunuo). Basi
“Waulizeni wenye kumbu kumbu(za vitabu vya Allah vya kale) ikiwa nyinyi hamjui”.
(An-nahl:43)
بِٱلْبَيِّنَٰتِ وَٱلزُّبُرِ ۗ وَأَنزَلْنَآ إِلَيْكَ ٱلذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ
(Tuliwaleta)Kwa Ishara zilizowazi na Vitabu. Na Tumekuteremshia mawaidha ili uwabainishie watu yaliyateremshwa kwao, na ili wapate kufikiri.
(An- nahl:44)
Ndani ya ayah hii, Allaah -jalla wa’alaa- ameamrisha washirikina katika makafiri wa kiqurayshi na wengineo, wawaulize wajuzi, yaani wale waliopewa kitabu, kuhusu je, Mtume aliyewajia wao ni mtu au ni malaika?
Na ikionekana kuwa Mtume aliyewajia wao ni mtu, basi kubalini ujumbe aliokuja nao Muhammad (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) , kwasababu yeye ni mtu ambaye walishapita kabla yake Mitume.
Na wamesifiwa ahlul-kitabi kuwa wao ni watu wa dhikri (wajuzi), kwasababu kitabu ambacho amekiteremsha Allaah -jalla wa’alaa- ni dhikri.
Na dhikri iliyojuu kabisa ni Al-Qur’aan , kama alivyosema Allaah (subhaanah!):
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا ٱلذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَٰفِظُونَ
Hakika Sisi ndio tulio teremsha mawaidha haya, na hakika Sisi ndio tutakao yalida(Al- hijr:9).
“Hakika sisi Tumeiteremsha dhikri, na hakika sisi tutaihifadhi”.
Na amesema Allaah-jalla wa’alaa- katika ayah hizi:
وَمَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِىٓ إِلَيْهِمْ ۚ فَسْـَٔلُوٓا۟ أَهْلَ ٱلذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ بِٱلْبَيِّنَٰتِ وَٱلزُّبُرِ ۗ وَأَنزَلْنَآ إِلَيْكَ ٱلذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ (النحل: 43-44)
Wamesema Wanazuoni:
Ayah hii imeshuka katika kuwauliza ahlul-kitabi, lakini kuenea kwa lafudhi yake (العموم) kuna shamili kuwauliza pia watu wa Qur’aan na Sunnah. Kwasababu wao wana haki zaidi ya kubainisha yale aliyoyateremsha Allaah -jalla wa’alaa- , na ndio maana akasema:
وَأَنزَلْنَآ إِلَيْكَ ٱلذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ
“Na Tumekuteremshia dhikri( mawaidha) ili uwabainishie watu yale yaliyoteremshwa kwao”.
Amesema Shaykh ‘Abdur-Rahman bin Sa’diy katika “tafsiir” yake kwenye ayah hii:
وعموم هذه الأية فيها مدح أهل العلم، وأن أعلى أنواع العلم، العلم بكتاب الله المنزل، فإن الله جل وعلا أمر من لم يعلم بالرجوع إلى أهل العلم وأهل الذكر في جميع الحوادث
“Na kuenea kwa ayah hii, ndani yake kuna kusifiwa kwa Wanazuoni, na kwamba aina ya juu kabisa ya elimu ni elimu ya kukijua kitabu cha Allaah kilichoshushwa. Kwasababu Allaah- jalla wa’alaa- , amemuamuru asiyejua kurejea kwa Wanazuoni na watu wa dhikri katika mambo yote.
Na pia katika hilo kuna ta’diil kwa Wanazuoni na kuwasifu. Pale alipoamuru Allaah kuulizwa wao , na kwa hilo (la kuwauliza wao) mtu mjinga atatoka kwenye orodha ya ufuasi.
Hakika asili (ya hilo) ipo katika kitabu cha Allaah, na kwamba mtu asipojua kitu , na kushindwa kujua hekima yake anatakiwa kuwauliza Wanazuoni.
Na anapowauliza Wanazuoni wajuzi wa kitabu na sunnah ambao imekita miguu yao na kuimarika katika hilo, hakika ufuasi wake (wa yeye kuwa katika wajinga) unaondoka. Kwasababu amewauliza aliotakiwa na Allaah-jalla wa’alaa- awaulize.
Hivyo yeyote asiye na elimu ya kitu fulani, kisha akaulizia kuhusu hukumu yake (kitu hicho), akamuuliza ‘Aalim mwenyethabati, hakika ufuasi wake unaondoka .
Na akilifanyia kazi lile alilojuzwa, basi humuondoka yeye dhima (madhuur), kwasababu amelifanyia kazi aliloamrishwa na Allaah -jalla wa’alaa- kwenye kauli yake:
“Waulizeni wajuzi ikiwa hamjui”.
Muhusika: Shaykh Swaalih Aalish-Shaykh
Mtarjimu:duaatsalaftz.net
Marejeo: adabus-suaal uk.12
Imehaririwa: 19’jumaadal-uwlaa/1438H.