14. Hivyo , miongoni mwa adabu ni kutouliza kwa Wanazuoni wengi


Kwasababu wingi wa maswali
1: unabana nyakati za Wanazuoni
2: utamuweka muulizaji kwenye matatizo, na wengi wa waulizao husikika wakisema:
“Tumebaki njia panda hatujui kipi cha kufanya, huyu asema hivi na yule asema vile!
Tunakwambia (wewe mwenye tabia hiyo):
Wewe ndiye mkosa namba moja pale ulipowauliza Wengi katika Wanazuoni, ulipaswa umuulize mmoja unayemuamini kwa elimu yake na Dini yake, kisha chukua fat’wa yake , na ujitakase mbele ya Allaah -jalla wa’alaa- . Kwasababu Allaah -jalla wa’alaa- amekuamuru uwaulize Ahludh-Dhikr na umeshatekeleza hilo na umewauliza hivyo usiizidishie nafsi yako mzigo mzito.
Muhusika: Shaykh Swaalih Aalish-Shaykh
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: adabus-suaal uk.20
Imehaririwa: 24’jumaadal-uwlaa/1438H