15. Kuuliza swali kwa uwazi bila ya kufumbia wala hakuna haya kwenye kuuliza mambo ya Dini


Miongoni mwa adabu ni usiulize swali kwa kulibanabana au kwa mafumbo.
Mfano:
Wapo baadhi ya watu wanauliza kwa kusema:
Fulani katika watu alipatwa na kadha wa kadha!
Lakini lengo lake (huyu muulizaji) ni kutaka kujinasua kwenye mambo yanayomuhusu yeye lakini kwa njia ya kuyafananisha, ilhali akiwa anadhani ya kwamba kama atajibiwa (suala la fulani) basi utatuzi huo pia utakuwa ni utatuzi wa jambo lake.
Utamkuta anasema (mathalan):
Fulani lau angepatwa na jambo fulani au fulani….!!
Ilhali suala lake (ambalo analisubiria jawabu kupitia kadhia inayomuhusu fulani) linatofautiana na tukio la huyo fulani anayemuulizia.
Lakini yeye anadhani kwamba lake na la fulani ni sawa, kusudio lake asijulikane na ‘Aalim kwamba yeye ndiye aliyetenda jambo hilo, akawa anahitajia jawabu lakini kwa swali la ujanja.
Muhusika: Shaykh Swaalih Aalish-Shaykh
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: adabus-suaal uk.21
Imehaririwa: 24’jumaadal-uwlaa/1438H