16. Kuwauliza Wanazuoni hakuna haja ya kuona aibu bali ni hadhi


Kuwauliza Wanazuoni ni hadhi na sharaf, na ni dalili juu ya pupa ya muulizaji katika kheri na kutaka kwake kujinasua na kujitoa katika dhima fulani.
Na pia hilo linamfanya akhafifishe hali ya ufuataji mkumbo mpaka pale atakapokutana na Mola wake -jalla wa’alaa-:
Hivyo itokeapo unauliza swali kwa Wanazuoni usiulize kwa kulibana swali bali uliza kwa uwazi kabisa na wala hakuna dhambi juu ya hilo.
Walishauliza baadhi ya maswahaba wa kike kuhusu hukumu ya mwanamke aliyeona majimaji baada ya mwanamke kuota (anaingiliwa) ni ipi hukumu yake!?
Na haya haipatikani katika kuuliza kwasababu haya ni jambo lenye kuhimidiwa.
Lakini haya haitokuwa mahmuud (yenyekuhimidiwa) itakapokuwa inakuweka mbali na maarifa ya kutambua hukumu za Dini, haya hiyo haitokuwa nzuri kama ilivyokuja katika hadithi.
Muhusika: Shaykh Swaalih Aalish-Shaykh
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: adabus-suaal uk.21
Imehaririwa: 24’jumaadal-uwlaa/1438H