17. Hivyo, katika adabu ambazo inatupasa kuzichunga ni kuuliza swali ambalo unalihitajia


Na kwamwe usichukulie kuwa wewe utakapolifumba swali kisha (‘Aalim) akajibu ,usidhani kuwa jawabu litaendana na swali lako.
Lau ungemuuliza kwa uwazi kabisa bila shaka jawabu lisingekuwa hilo alilokupa baada ya kuuliza kwa kufumba.
Hivyo usiwe unafumba unapowauliza Wanazuoni.
Si katika masuala ya kifiqhi wala yanayohusu kutaka kujua watu fulani na hali fulani.
Bali itapasa swali liwe wazi, na hilo la kuweka swali kwa uwazi ni miongoni mwa heshima kwa Wanazuoni na kupupia kupata jawabu stahiki.
Ama masuala ya kuwafumbia Wanazuoni kisha kutaraji kutoka kwao majibu ya sawa sawa hili haliendani kabisa na kuwatukuza Wanazuoni, na pia haliondoshi dhima yako kwasababu utamtelezesha ‘Aalim katika kujibu. Na lau angejua swali kwa uhakika wake na muradi wako huenda akatoa jawabu jengine hivyo bado kwa uulizaji wa kufumbia hujajitakasa dhima.
Hivyo tunaonelea kwamba matatizo mengi ya kugongana kwa kauli za baadhi ya Wanazuoni katika baadhi ya masuala ya kifiqhu au masuala yanayojiri pamoja na masula ya kijamii na mfano wake chanzo chake ni aina kama hii ya uulizaji wa kufumbia mambo, na jambo hili halifai kwasababu Allaah -jalla wa’alaa- ametuamrisha tuulize kwa uwazi , na huyu muulizaji akalikiuka hili.
بتصرف
Muhusika: Shaykh Swaalih Aalish-Shaykh
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: adabus-suaal uk.23
Imehaririwa: 28’jumaadal-uwlaa/1438H