18. Usimuulizie mtu mwengine


Miongoni mwa adabu ambazo inapaswa kuchungwa wakati wa uulizaji ni kuwa muulizaji anauliza kwa niaba ya nafsi yake mwenyewe na wala hamuulizii mwengine.
Mara nyingi huja maswali muulizaji anauliza:
Mmoja wa jamaa zangu wa karibu ameniomba nimuulizie kuhusiana na kadhaa wa kadhaa!
Au utamkuta anasema:
Lau ikitokea kwa fulani -ambaye ni mfanyakazi mwezangu- amepatwa na kadhaa wa kadhaa na ameniomba nimuulizie.
kwanini asiulize mwenyewe!?
Huoni kuwa hali zitatofautiana! kwasababu ‘Aalim lazima aulize na apambanuliwe swali.
Atauliza kwa mfano:
Kulitokea nini!?
Je hiki nacho kilitokea!?
Sasa muulizaji akiwa si yule aliyetokewa na jambo hawezi kutoa msaada wa kutolewa kwa jawabu, labda iwe katika mazingira ya kuwa swali ni fupi na kilichomzuia aliyetokewa na hilo jambo asiulize mwenyewe ni haiba yake kumchelea ‘Aalim au kumuona haya kwa mazingira yanayoruhusiwa.
Kama alivyofanya ‘Aliyy bin Abiy Twalib (Allaah amridhie), alikuwa sana hutokwa na Madhii, na akaona haya kumuuliza Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) kwa nafasi aliyokuwa nayo bint yake kwake. Yaani kwaajili ya Faatwimah kuwa ni mke wa Aliyy, akaogopa kuuliza na akapatwa na haiba kuuliza swali kama hili ambalo linahusu mambo ya tupu. Akamtuma Miqdaad (Allaah amridhie) akamuulize Nabiyy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) kuhusu jambo hili la kutokwa na madhiy kwa wingi. Akamuuliza kisha Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) akatoa jibu kisha jawabu likamfikia ‘Aliyy (Allaah amridhie).
Hivyo, asili ni kwamba kila mtu aulize yanayomuhusu, kwasababu majibu yatatofautiana kulingana na hali ya muulizaji na jinsi anavyouliza.
Na yule anayeuliza swali kwa kunukuu mara nyingi hawezi kutoa taswira ya swali kwa uhakika wake.
Na mara nyingi hutoka majibu kwa hali isiyo salama kwasababu kama hizi za uulizaji kama humu.
بتصرف يسير
Muhusika: Shaykh Swaalih Aalish-Shaykh
Mtarjimu: duaatasalaftz.net
Marejeo: adabus-suaal uk.24
Imehaririwa: 28’jumaadal-uwlaa/1438H