63. Thawabu za kufanya lindo (doria) katika njia za Allaah-‘azza wajalla-


 

ثواب الرباط في سبيل الله عز وجل

عن عثمان بن عفان رضي الله عنه يقول:  سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول:  ((رباط يوم في سبيل الله خير من ألف يوم فيما سواه من المنازل)).

Imepokelewa kutoka kwa ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Allaah amridhie) amesema:
Nimemsikia Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) akisema:
“Lindo la siku moja katika njia ya Allaah ni bora kuliko siku elfu moja katika ibada nyengine”.

رواه الترمذي وحسنه، وابن حبان، والحاكم، وقال: صحيح على شرط البخاري، وابن ماجة إلا أنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول:  ((من رابط ليلة في سبيل الله كانت كألف ليلة صيامها وقيامها)).

Ameipokea Al-Tirmidhiy na ameihasanisha. Na ameipokea pia Ibn Hibban na Al-Haakim, na akasema (Al-Haakim): Ni sahihi kwa shatri za Imam Bukhary.  Pia ameipokea Ibn Maajah isipokua kwake alisema hivi (‘Uthmaan):
Nimemsikia Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) akisema:
“Yeyote atakayekaa lindoni usiku mmoja katika njia ya Allaah,  (malipo yake) yatakuwa  sawa na swaum na kisimamo cha siku elfu moja”.

[صحيح: رواه النسائي (٤٠/٦)، والترمذي (١٦٦٧)، وابن حبان (٤٥٦٠)، والحاكم (٦٨/٢) ، وابن ماجة (٢٧٦٦)، وصححه الألباني في “المشكاة” (٦٨٣١)].

Sahihi: Ameipokea Al-Nasaaiy (6/40), na Al-Tirmidhiy (1667), na Ibn Hibban (4560), na Al-Haakim (2/68), na Ibn Maajah (2766), na ameisahihisha Al-Albaaniy katika “al-mishkaat” (6831).

وعن سهل بن سعد رضي الله عنه قال:  إن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:  ((رباط يوم في سبيل الله خير من الدنيا وما عليها)).

[صحيح: رواه البخاري (٢٨٩٢)، ومسلم (١٨٨١)].

Na imepokelewa kutoka kwa Sahl bin Sa’d (Allaah amridhie) amesema:

Hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Lindo la siku moja (tu) katika njia ya Allaah ni bora kuliko dunia na vilivyomo juu yake”.
Sahihi: Ameipokea Imam Bukhary (2892), na Muslim (1881).
Tanbii:
Wenye kufanya lindo hilo (doria) ni wale wenye kulinda mipaka isivamiwe na majeshi ya kikafiri, wanalinda mali za Waislam na heshima zao, wakati huo huo wapo tayari kwa uchache wao wa idadi kupambana na wavamizi hao.
Muhusika: Shaykh Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.19
Imehaririwa: 2’shab/1438H