75. Thawabu kwa Mwenyekutamka Shahada Mbili


ثواب من شهد أن لا إله إلا الله وأن محمدا رسول الله

عن عبادة رضي الله عنه، عن النبي صلى الله عليه وسلم قال : ((من شهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له، وأن محمدا عبده ورسوله، وأن عيسى عبد الله ورسوله وكلمته ألقاها إلى مريم وروح منه، والجنة حق، والنار حق، أدخله الله الجنة على ما كان من العمل)).
[صحيح: رواه البخاري (٣٤٣٥)، ومسلم (٢٨)]

Imepokelewa kutoka kwa ‘Ubaadah (Allaah amridhie) , kutoka kwa Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Yeyote atakayeshahadia (kwa kukiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi) kwamba hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki
ispokuwa Allaah pekee hana mshirika, na kwamba Muhammad ni mja wake na Mtume wake, na kwamba Issa ni mja wa Allaah na Mtume wake, na ni neno lake aliloliweka kwa Maryam na ni Roho itokayo kwake, na akashahadia kuwa pepo ni haki (ipo) na moto ni haki, ataingizwa peponi na Allaah juu ya amali nyengine alizokuwa nazo”.
Sahihi: Ameipokea Bukhary (3435), na Muslim (28).

وعن أنس بن مالك رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم ومعاذ رديفه على الرحل، قال: ((يا معاذ بن جبل!)).
قال:لبيك يا رسول الله وسعديك. ثلاثا، قال: ((ما من أحد يشهد أن لا إله إلا الله ، وأن محمدا رسول الله صدقا من قلبه إلا حرمه الله على النار)).
قال: يا رسول الله! أفلا أخبر بها الناس فيستبشروا؟ قال: ((إذا يتكلوا)).
[صحيح: رواه البخاري (١٢٨)، ومسلم (٣٢)]

Na imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Allaah amridhie) , kwamba hakika Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) alisema kumwambia Mu’aadh bin Jabal (Allaah amridhie) akiwa amempakiza juu ya mnyama (wake):
“Ewe Mu’aadh Mwana wa Jabal!”.
Akaitika: “Labbayk wasa’dayk ewe Mtume wa Allaah!”.
alisema hayo mara tatu.
akasema Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Hakuna yeyote atakayeshahadia kuwa hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah , na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, akiwa mkweli moyoni mwake isipokuwa Allaah atauharamisha juu yake moto”.
akasema (Mu’aadh):
“Ewe Mjumbe wa Allaah! kwa nini nisiwape watu khabari hii ili wafurahi!?”
akasema:
“Ukiwapa watazembea (wataacha kujituma katika ibada wategemee hilo”.
Sahihi: Ameipokea Bukhary (128), na Muslim (32).

 

Muhusika: Shaykh Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu : duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.23
Imehaririwa: 27’shab/1438H