77. Thawabu kwa atakayelitamka neno hilo (la Tawhiid) mara mia


ثواب من قالها في اليوم مائه مرة

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((من قال لا إله إلا الله وحده لا شريك له ، له الملك وله الحمد ، وهو على كل شيئ قدير في يوم مائة مرة، كانت له عدل عشر رقاب ، وكتبت له مائة حسنة، ومحيت عنه مائة سيئة، وكانت له حرزا من الشيطان يومه ذلك حتى يمسي ، ولم يأت أحد بأفضل مما جاء به إلا أحد عمل أكثر من ذلك)).
[صحيح: رواه البخاري (٣٢٩٣)، ومسلم (٢٦٩١)]

Imepokelewa kutoka kwa Abiy Hurayrah (Allaah amridhie) , kwamba hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Yeyote atakayesema: hakuna Mola apasayekuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, peke yake hana mshirika, ufalme ni wake na himid ni zake, na yeye juu ya kila kitu ni Muweza, kwa siku (akasoma hayo) mara mia moja, kwake yeye itakuwa ni sawa na kuwaacha huru watumwa kumi, na ataandikiwa mema mia moja, na atafutiwa makosa mia moja, na yatakuwa ni kinga kwake kutokana na shetani siku yake hiyo mpaka afikapo jioni, na wala hatopatikana yeyote atakayekuja na bora zaidi kumshinda yeye, ila yule ambaye atamzidi kwa idadi”.
Sahihi: Ameipokea Bukhar (3293), na Muslim (2691).

Tawdhiih:

atakayemzidi ni yule atakayemzidi kwa idadi , badala ya kusoma mara mia moja mathalan, akasoma mara mia moja na khamsini.

Muhusika: Shaykh Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.24
Imehaririwa: 27’shab/1438H