98. Thawabu katika kuwatendea wema wazazi wawili na kuwatii


 

 

◆ ثواب الوالدين وطاعتهما◆

وعن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: سألت رسول الله صلى الله عليه وسلم: أي العمل أحب إلى الله؟ قال: (( الصلاة على وقتها)) ، قلت: ثم أي؟ قال: ((بر الوالدين))

[صحيح: رواه البخاري (٥٢٧) ، ومسلم (٥٨)]
Imepokelewa kutoka kwa Abdillaah bin Mas’uud (Allaah Amridhie) amesema:
Nilimuuliza Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Ni amali ipi inapendeza mno kwa Allaah?”.
Akasema (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
→ ” Kuswali swala katika wakati wake”.

Nikamuuliza:

“Kisha amali ipi (baada ya hiyo)?”.

Akasema (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):

→ “Kuwatendea Wema wazazi wawili”.
Sahihi: Ameipokea Bukhariy (527) , na Muslim (58).

عن ابن عمر رضي الله عنهما أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((بينما ثلاثة نفر يتماشون أخذهم المطر فمالوا إلى غار في الجبل ، فانحطت على فم غارهم صخرة من الجبل فأطبقت عليهم ، فقال بعضهم لبعض: انظروا أعمالا عملتموها لله صالحة ، فادعوا الله بها لعله يفرجها. فقال أحدهم: اللهم! أنه كان لي والدان شيخان كبيران ولي صبية صغار كنت أرعي عليهم ، فإذا رحت عليهم فحلبت بدأت بوالدي أسقيهما قبل ولدي ، وإنه ناء بي الشجر فما أتيت حتى أمسيت فوجدتهما قد ناما ، فحلبت كما كنت أحلب فجئت بالحلاب فقمت عند رؤوسهما أكره أن أوقظهما من نومهما وأكره أن أبدأ بالصبية قبلهما ، والصبية يتغاضون عند قدمي فلم يزل ذلك دأبي ودأبهم حتى طلع الفجر ، فإن كنت تعلم أني فعلت ذلك ابتغاء وجهك فافرج لنا فرجة نرى منها السماء ، ففرج الله لهم فرجة حتى يرون منها السماء)). قلت: فذكر الحديث

[صحيح: رواه البخاري (٣٤٦٥) ، ومسلم (٢٧٤٣)]
Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Umar (Allaah awaridhie) , kwamba hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Kipindi walipokuwa watu watatu wakitembea , ghafla walinyeshewa na mvua , wakaingia kwenye pango lililopo katika jabali (kujificha mvua). Likadondoka jiwe kutoka juu likaziba uwazi wa pango walioingilia. Wakaambizana (baada ya kuona hali hiyo):
Tizameni (katika kumbukumbu zenu) matendo mema mliyoyatenda kwaajili ya Allaah kwa Ikhlaas , kisha muombeni Allaah kupitia matendo hayo huenda Allaah akaliondoka jiwe hilo.

Akasema mmoja wao:

Ewe Allaah! Hakika hali na shani jinsi ilivyo , Mimi nilikuwa na wazazi wangu wawili watuwazima vikongwe , na nilikuwa na watoto wangu wadogo , wote hao wapo chini ya uangalizi wangu (kinafaqa) , ninaporudi na wanyama wangu (toka malishoni) kisha nnapowakamua maziwa huanza kuwanywesha kwanza wazazi wangu wawili kabla ya watoto wangu. Na hakika siku moja nilikwenda kwenye malisho ya mbali kabisa mpaka nikachelewa na kurudi wakati wa usiku, nikawakuta (wazazi wangu wawili) wameshalala , nikakamua maziwa kama kawaida yangu kisha nikaja na chombo cha kukamulia Maziwa kwa wazazi wangu (wakiwa wamelala) nikawasimamia upande walioweka vichwa vyao huku nikichukia tendo la kuwaamsha kuwatoa usingizini mwao , na wakati huo huo nachukia tendo la kuanza kuwanywesha watoto kabla ya wazazi. Ilhali watoto wananipigia zogo chini ya miguu yangu , haikuachakuwa hiyo ndiyo hali yangu baina yangu na wao mpaka ikachomoza alfajr.
Basi (ewe Allaaah!) kama unajua kwamba mimi nimelifanya hilo kwa lengo la kuutaka USO wako (kuuona siku ya kiyama niwe katika walioridhiwa na wewe), basi tupe upenyu ambao kwa upenyu huo tutaweza (angalau) kuiona mbingu”.

Nimesema (Shaykh Ikhtiyaar):

Akamalizia kuitaja hadithi mpaka mwisho wake.
Sahihi: Ameipokea Bukhariy (3465) , na Muslim (2743).

وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنه قال: أقبل رجل إلى نبي الله صلى الله عليه وسلم فقال: أبايعك على الهجرة والجهاد أبتغي الأجر من الله. قال: (( فهل من والديك أحد حي؟؟ )). قال: نعم بل كلاهما. قال: ((فتبتغي الأجر من الله؟)). قال: نعم. قال: ((فارجع إلى والديك فأحسن صحبتهما))

رواه البخاري ومسلم وأبو داود إلا أنه قال: جاء رجل إلى رسول الله صلى الله عليه وسلم فقال: جئت أبايعك على الهجرة وتركت أبوي يبكيان ، فقال: ((إرجع عليهما فأضحكهما كما أبكيتهما))
[صحيح: رواه البخاري (٢٠٠٤) ، ومسلم (٢٥٤٩)]
Na imepokelewa kutoka kwa ‘Abdillaah bin ‘Amri bin Al-‘Aasw (Allaah awaridhie) amesema
Alikuja bwana mmoja kwa Nabii wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) akasema:
Ninakupa kiapo cha utiifu juu ya hijrah (kuhama kwaajili ya Allaah) , na Jihaad (katika njia ya Allaah) , huku nikiwa nataraji malipo kutoka kwa Allaah.
Akasema (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Je, una yeyote katika wazazi wako aliyehai?”.
Akajibu (Allaah amridhie):
Ndiyo. Bali wote (wapo hai).
Akasema (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Unataka ujira kutoka kwa Allaah?”.
Akajibu (Allaah amridhie):

Ndiyo.

Akasema (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):

” Rudi kwa wazazi wako (wawili) kakae nao kwa Wema”.

Ameipokea Bukhariy , Muslim na Abuu Daud , isipokuwa katika mapokezi ya Abuu Daud mpokezi alisema hivi:
“Alikuja bwana mmoja kwa Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) Akasema:
Nimekuja kukupa kiapo cha utiifu (bay’ah) , juu ya kufanya hijrah , lakini nimewaacha wazazi wangu wawili wanalia.
Akasema (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Rudi kwao , na uwachekeshe kama ulivyowaliza”.
Sahihi: Ameipokea Bukhariy (2004) , na Muslim (2549).

🌼 Faida🌼

1.Katika hadithi ya kwanza imetuonesha kuwa kuwatendea Wema wazazi wawili amali hiyo ni katika bora za amali. Bali jambo hilo ni haki yapili baada ya haki ya Muumba na Mtumewe (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam).
2.Amejaalia Mtume wetu (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) daraja la kuwatendea Wema wazazi limetangulia kuliko daraja la kupigana Jihaad katika njia ya Allaah.
3.kama atauliza Mtu , nini maana ya Al-Birr? (kwa wazazi).

Tutamjibu:

Ni wema kuwafanyia wa maneno na matendo na kuwapa mali kwa kadri ya uwezo.

Ibn ‘Uthaymiin (Allaah amraham).

🔘 faida:🔘

Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) anamuombea dua mbaya yule MTU ambaye amewadiriki wazazi wake wote wawili au mmoja wao akiwa hai, kisha mzazi wake asiwe sababu ya yeye kuingia peponi.
⭕ Kadhalika akatahadharisha Mtume wetu (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) juu ya kuwafanyia utovu wa nidhamu wazazi wawili akasema;
“Mambo mawili hutangulizwa malipo yake hapa duniani kabla ya akhera, dhulma na utovu wa nidhamu kwa wazazi wawili”.
Mtu dhalimu hafi kwa kheri. Na mtovu wa nidhamu kwa wazazi atalipwa kwa kufanyiwa hayo hayo amfanyiayo mama au baba yake na wanawe.
Allaah ametuadabisha kwa hali za uzee wafikiazo wazazi wetu na gubu la utuuzimani , na pamoja na yote hayo akatukataza tusiwasonye wala kuwanyusa na kuguna.
Bali tusiinue sauti zetu mbele ya sauti zao , wala tusiwakemee.
Bali ametutaka tuongee nao kwa maneno ya ukarimu na kuwaombea dua hata kama wapo hai.

Mwisho inapaswa tuelewe kuwa:

⭕ “Radhi za Allaah zipo sanjari na radhi za wazazi wawili , na ghadhabu zake zipo sanjari na ghadhabu za wazazi wawili”.
✍🏽 Ameihasanisha Imam Al-Albaaniy.

Muhusika: Shaykh ‘Ubayd

Kiunganishi: http://duaatsalaftz.net/category/makala/miirathun-nabiyy/
Mtarjim:http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: miiraathun-Nabiyy Uk.32
Imehaririwa: 21’J-Uwlaa/1439H