01.Tawhiidul-Twalab Wal-Qasd (Tawhiidul-Uluuhiyyah)


Maana ya Tawhiidul-Uluuhiyyah:

Tawhiidul-Uluuhiyyah:  Ni kumpwekesha Allāh  kwa kumuabudu peke yake  bila ya kumshirikisha.

Njia za Qur’an katika kujenga hoja juu ya Tawhiidul-Uluuhiyyah:

Qur’an imejenga hoja  juu ya uwajibu  wa kumpwekesha Allāh  katika ibada kupitia Tawhiidul-Rubūbiyyah na Tawhiidul-Asmāi Wasswifāt.   Kwa ile talaazum iliyopo baina ya aina za Tawhiid.

Kwani hakutokuwa na Mola anayestahiki kuabudiwa peke yake ila yule ambaye ni Muumba, mwenye kuruzuku, mwenye kumiliki na mwenye kuleta mabadiliko na mwenye kuweza kuyaendesha mambo, aliye hai, mwenye kujisimamia na kuwasimamia walimwengu, msikivu mwenye kuona, mwenye ujuzi na mwenye hekima, aliyemkwasi asiyehitaji kutoka kwa yeyote, aliyetakasika kutokana na kila sifa pungufu na aibu, anayetegemewa na vyote, mtendaji mwenye kulichagua atakalo, asiye na wakumpinga katika hukumu zake, na wala mwenye kuzirudisha  kadhaa zake, asiyeshindwa na kitu mbinguni na ardhini, asiyepitwa na kitu mbinguni wala aridhini, na wala hakifichiki chochote juu yake kwani amevizunguka vitu vyote kwa elimu.

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah

Kiunganishi:  http://duaatsalaftz.net/category/makala/kitaabu-tawhiidil-ibaadah/

Mtarjim:  http://duaatsalaftz.net/

Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah

Imehaririwa: ‘6Jumaadal-Thāniy/1440H