05.Hakika ya Tawhiid-Ilāhiyyah (Al-‘Ibādah)


1. Tawhiid ni haki ya Allāh  iliyopo juu ya waja wake, wamuabudu peke yake na wasimshirikishe. Ama haki ya waja iliyopo kwa Allāh  ni kutomuadhibu ambaye hatamshirikisha na chochote. Kama alivyosema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) katika hadithi ya Mu’ādh (Allāh  amridhie):

فإن حق الله على العباد أن يعبدوه ولا يشركوا به شيئا، وحق العباد على الله أن لا يعذب من لا يشرك به شيئا

رواه الشيخان

“Hakika haki ya Allāh  iliyopo juu ya waja ni wampwekeshe katika Ibada na wasimshirikishe na chochote, na haki ya waja kwa Allāh  ni kutomuadhibu asiyemshirikisha na chochote”.

Ameipokea Bukhari na Muslim.

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah

Kiunganishi: http://duaatsalaftz.net/category/makala/kitaabu-tawhiidil-ibaadah/

Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/

Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah

Imehaririwa: ‘6Jumaadal-Thāniy/1440H