06.Hakika ya Tawhiid Al-Ilāhiyyah (Al-Ibādah)


2. Ni Tawhiid ambayo Allāh  amewatuma kwa ajili yake Mitume wake wote (‘Alayhimus-Salām) wakilingania juu yake.

Kama alivyosema Allāh  Mtukufu:

“وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُون”ِ  الأنبياء (25)

“Na hatujamtuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa tulimshushia Wahyi kuwa hakuna Mola anaepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa mimi basi nipwekesheni katika Ibada”. An-Biyaa (25).

Na amesema Allāh  Mtukufu:

“وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ ” النحل (٣٦)

“Na kwa hakika Tumetuma katika kila Ummah Mtume awaambie muabuduni Allāh  na jiepusheni na twāghuut” Al-Nahl (36).

Na kila Nabiy aliwaambia watu wake:

“اعْبُدُوا اللَّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَٰهٍ غَيْرُهُ ۖ ” الأعراف (٥٩)

“Mpwekesheni Allāh  katika Ibada kwani hamna  nyinyi Mola mwengine asiyekuwa yeye” Al-A’rāf (59).

Na amesema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam), kama ilivyokuja katika hadithi ya Abū Hurayrah (Allāh amridhie):

“والأنبياء إخوة لعلات أمهاتهم شتى ودينهم واحد”

رواه الشيخان

ومعنى إخوة لعلات: هم الإخوة لأب من أمهات شتى

“Na Manabii ni ndugu wenye mama tofauti ila  Dini yao ni Moja”

Ameipokea Bukhari na Muslim.

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah

Kiunganishi: http://duaatsalaftz.net/category/makala/kitaabu-tawhiidil-ibaadah/

Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/

Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah

Imehaririwa: ‘6Jumaadal-Thāniy/1440H