08.Hakika ya Tawhiid Al-Ilāhiyyah (Al-Ibādah)


  1. Aina hii ya Tawhiid ndio ambayo Allāh (Mtukufu) amemuamrisha Mtume wake Muhammad (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) apambane (Jihad) na wale watakaokwenda kinyume nayo. Kama alivyosema Allāh  Mtukufu:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ جَاهِدِ الْكُفَّارَ وَالْمُنَافِقِينَ وَاغْلُظْ عَلَيْهِمْ ۚ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ  ” التوبة (73

“Ewe Nabii! Pigana Jihadi na makafiri na wanafiki na kuwa mkali juu yao, na maishilio yao ni Jahanam na hayo ni marejeo mabaya kabisa”.  Al-Tawbah (73).

Na amesema Allāh  Mtukufu:

وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّهِ ۚ         ” البقرة  (١٩٣

“Na pambaneni nao mpaka itoweke shirki na ibaki Dini kuwa ni ya Allāh”. Al-Baqarah (193).

Na amesema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam):

“Nimeamrishwa nipambane na watu mpaka washahadie kuwa;

لا إله إلا الله

Na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allāh, na wasimamishe swala na watoe zaka. Wakiyafanya hayo wanazikinga kutokamana nami damu na mali zao isipokuwa kwa haki ya Uislam na hesabu yao ipo kwa Allāh”

Ameipokea Bukhari na Muslim kutoka kwa hadithi ya Ibn ‘Umar (Allāh  awaridhie).

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah.

Kiunganishi: http://duaatsalaftz.net/category/makala/kitaabu-tawhiidil-ibaadah/

Mtarjim:http://duaatsalaftz.net/

Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah