11.Fadhila na ubora wa Tawhiid- B


Ni kwamba yeyote atakayeipatikanisha hii Tawhiid (maishani mwake) itakingwa damu yake na kuhifadhiwa Mali yake Ila kwa haki yake. Kama alivyosema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam):

من قال لا إله إلا الله وكفر بما يعبد من دون الله حرم ماله ودمه وحسابه على الله

رواه مسلم

“Yeyote atakayesema:

لا إله إلا الله

Na akawakanusha wote wanaoabudiwa kinyume na Allāh basi itaharamishwa mali yake na damu yake na hesabu yake ipo kwa Allāh”.
Ameipokea Muslim.

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah