12. Makemeo kwa waasi wa wenye Tawhiid kuingia motoni


Hadithi zilizokuja kusema kuwa yeyote atakayetamka:

لا إله إلا الله

Ataingia peponi, au kuwa Allāh  amemharamishia moto mtu  huyo, hizo hazipingani na hadithi zilizokuja kwa makemeo. Kama yalivyo  maneno yake Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) katika hadithi ya Abdillāh bin ‘Amr (Allāh  amridhie):

“من شرب الخمر وسكر لم تقبل له صلاة أربعين صباحا وإن مات دخل النار”

رواه ابن ماجة (صحيح)

” Yeyote atakayekunywa pombe na kulewa haitokubaliwa swala yake kwa muda wa siku arubaini, na kama atakufa basi ataingia motoni.
Ameipokea Ibn Mājah (sahihi).
Na  njia za kuzijumuisha hadithi hizo (zinaonesha kusigana) nikama ifuatavyo:

 

  1. Baadhi ya ‘Ulamaa wamesema:
Muradi wa hadithi za shahada ya:

لا إله إلا الله

Ni kwamba huwa sababu ya kuingia peponi na kuokoka kutokana na moto na huo ni muktadha wake.
Pamoja ya kuwa muktadha huo hautofanya vyema kazi yake ila  kwa kutimia kwa sharti zake na kuondoka kwa vizuizi vyake.
Hivyo, muktadha huenda usifanye kazi kwa kukosekana kwa sharti moja miongoni mwa shuruti zake au kwa kupatikana kizuizi.
Na hii ni kauli ya Al-Hasan na Wahb bin Munabbih (Allāh  awarham).
  1. Ni kwamba ataharamishiwa moto kwa maana ya hatokaa milele humo. Na hilo ni pale atakapotaka Allāh  kumuadhibu kwa kosa lake alilolitenda, kisha atamtoa humo na kumuingiza peponi.  Kama alivyosema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam), katika hadithi ya Anas bin Mālik (Allāh amridhie):

“وعزتي وجلالى وكبريائي وعظمتي لأخرجن منها من قال لا إله إلا الله”

رواه الشيخان

“Naapa kwa Nguvu zangu, Utukufu wangu, Kiburi changu na Taadhima yangu! Hakika nitamtoa humo kila aliyesema:

لا إله إلا الله

Ameipokea Bukhari na Muslim.
Nimesema:
Na hilo ni kuwa watu wa Tawhiid katika wale waliokosea ambao Allāh  ametaka kuwaadhibu (kwa mujibu wa makosa yao) wao hawatokaa milele kwenye moto.  Bali huenda Allāh  akamsamehe atakayetaka  kumsamehe akamuingiza peponi bila ya kumuadhibu.

 

  1. Au ataharamishiwa moto kuingia tena  baada ya kuwa ameshatoka  humo.
Na kwa ujumla ni kwamba atakayesema:

لا إله إلا الله

Akaipatikanisha Tawhiid (maishani mwake), huyo atakuwa kama alivyosema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam), katika hadithi ya Abū Hurayrah (Allāh  amridhie):

“من قال لا إله إلا الله نفعته يوما من دهره يصيبه قبل ذلك ما أصابه”

رواه البزار (صحيح)

“Yeyote atakayetamka:

لا إله إلا الله

Litamnufaisha neno hilo siku moja, hata kama kabla ya hapo alifanya madhambi  maishani mwake yale aliyoyafanya”.
Ameipokea Al-Bazzār (sahihi).

والله أعلم

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah