14. Maana ya Shahādah


Maana ya Shahādah ya

لا إله إلا الله

Ni hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allāh.
Nguzo za Shahādah ya

لا إله إلا الله

Ina nguzo mbili:
  1. Kukanusha
  2. Kuthibitisha.
Kukanusha (لا إله), hukanusha vyote viabudiwavyo kinyume na Allāh, hivyo hastahiki Ibada asiyekuwa yeye.
Kuthibitisha (إلا الله) , huthibitisha Ibada zote kwa Allāh  peke yake.
▪ Hivyo neno لا إله إلا الله
Ndani yake kuna herufu (لا), ambayo kazi yake hukanusha jinsi nzima (ya kila kinachokanwa).
Pia kuna (إله), hii ni ismu ya (لا), imejengwa juu ya fat’ha katika mahali pa nasbu. Na khabar ya (لا), imehadhifiwa na hukadiriwa kwa (حق), au (مستحق للعبادة).
Na dalili kuwa khabari hukadiriwa kwa kusema (haki) au (anayestahiki kuabudiwa), ni kauli yake Allāh  Mtukufu aliposema:

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ هُوَ الْبَاطِلُ

 الحج (٦٢)

“Hilo ni kwakuwa Allāh  ndiye wa haki na wale wanaowaomba kinyume chake ni batili”. Al-Hajj (62).

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah