22. Miongoni mwa Fadhila na Ubora wa Tawhiid- 8


Ndio tawi la  juu kabisa miongoni mwa matawi ya mti wa Iymān.  Kama alivyosema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) katika hadithi ya Abū Hurayrah (Allāh  amridhie):

“الإيمان بضع وسبعون أو بضع وستون شعبة فأفضلها قول لا إله إلا الله وأدناها إماطة الأذى عن الطريق والحياء شعبة من الإيمان”

“Iymān ni sehemu sabini na ziada, au sitini na ziada, sehemu iliyobora kabisa ni kusema لا إله إلا الله , na sehemu iliyoduni kabisa ni kuusogeza udhia kuutoa  njiani, na haya (aibu) ni sehemu katika Iymān”.

رواه مسلم، وفي لفظ

Ameipokea Muslim: na imekuja pia kwa lafudhi ya:

” الإيمان بضع وسبعون بابا أدناها إماطة الأذى عن الطريق  وأرفعها قول لا إله إلا الله”

رواه الترمذي (صحيح)

“Iymān ina milango sabini na ziada, ulio chini kabisa ni (tendo la) kuusogeza udhia kuutoa  njiani, na ulio juu kabisa ni kusema لا إله إلا الله “.
Ameipokea Al-Tirmidhiy (Sahihi).

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah