25. Miongoni mwa Fadhila na Ubora wa Tawhiid-11


Atakayesema:

لا إله إلا الله وحده لا شريك له

Bila shaka atayapata malipo yaliyokuja katika hadithi ya Abū Hurayrah (Allāh amridhie), ambayo ni kauli yake Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam):

من قال لا إله إلا الله وحده لا شريك له، له الملك وله الحمد وهو على كل شيئ قدير في يوم مائة مرة كانت له عدل عشر رقاب وكتبت له مائة حسنة ومحيت عنه مائة سيئة وكانت له حرزا من الشيطان يومه ذلك حتى يمسي ولم يأت أحد بأفضل مما جاء به إلا أحد عمل أكثر من ذلك

رواه الشيخان

“Yeyote atakayesema:

لا إله إلا الله وحده لا شريك له، له الملك وله الحمد وهو على كل شيئ قدير

“Hakuna Mola apasayekuabudiwa kwa haki ila  Allāh, peke yake hana mshirika, ufalme wa vyote ni wake, na himdi  zote anastahiki yeye, na yeye juu ya kila kitu ni Muweza”
Mara mia moja, hayo kwake yatakuwa ni sawa na kuwaacha huru watumwa kumi, na ataandikiwa mema mia moja, na atafutiwa mabaya mia moja, na hayo yatakuwa ni kinga kwake kutokana na shetani siku yake hiyo mpaka aingiwe na jioni, na hatotokea yeyote atakayekuwa bora zaidi kwa mtu huyo kwa lile alilolifanya ila ni yule atakayezidisha (idadi ya hiyo dhikri)”.
Ameipokea Bukhari na Muslim.

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah