29. Shuruti za لا إله إلا الله


{Sharti ya kwanza}

  1. Kuijua maana yake kwa hali yake ya kukanusha na kuthibitisha (نفيا وإثباتا). Elimu ambayo inapingana na ujinga.
Anatakiwa ajue (mja) kuwa hakuna mola anayestahiki kuabudiwa ila  Allāh.  Kama alivyosema Allāh  Mtukufu:

فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا اللَّهُ ” محمد (١٩)

“Basi jua kwamba hakika hakuna mola anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah” Muhammad (19).
Na kama alivyosema Allāh  Mtukufu:
“إِلَّا مَن شَهِدَ بِالْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ” الزخرف (86)
“Isipokuwa wale walioishuhudia haki (لا إله إلا الله) ilhali wanajua” Zukhruf (86).
Na amesema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam), kama ilivyokuja katika hadithi ya ‘Uthmān (Allāh  amridhie):

“من مات وهو يعلم أنه لا إله إلا الله دخل الجنة”

رواه مسلم

“Yeyote atakayekufa ilhali ana elimu juu ya لا إله إلا الله ataingia peponi”.
Ameipokea Muslim.

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah