01-04. Utangulizi


بسم الله الرحمن الرحيم

الحمد لله الذي رضي لنا الإسلام دينا، وأتم علينا النعمة وإكمل لنا الدين، وأشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له ، الملك الحق المبين، وأشهد أن محمدا عبده ورسوله الذي بعثه الله رحمة للعالمين، فأدى الأمانة ونصح الأمة وبلغ البلاغ المبين، اللهم صل وسلم وبارك عليه وعلى آله وأصحابه ومن سلك سبيله واهتدى بهديه إلى يوم الدين

                        Himdi zote zinamstahiki Allāh ambaye ameridhia Uislam kuwa ni Dini yetu, na akazitimiza juu yetu neema, na akatukamilishia Dini.  Na nakiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kuwa hakuna mola anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allāh, peke yake hana mshirika, mfalme wa haki aliye wazi.  Na nakiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kuwa Muhammad ni mja wake na Mtume wake, ambaye Allāh amemtuma kuwa ni Rahma kwa walimwengu wote, naye akatekeleza amana na akaunasihi ummah na akafikisha ufikisho wa wazi kabisa.
                       Ewe Allāh! Mswalie na umsalimu na mbariki pamoja na jamaa zake na Swahaba zake na kila atakayeifata njia yake na kuongoka kwa muongozo wake mpaka siku ya malipo.

Ama baada ya yaliyokwisha kupita.

                         Hakika kipindi kirefu nilikuwa na pendekezo la  kuandika sharh yenye kujitegemea inayohusu hadithi ya Jibriil (‘alayhis-salaam) iliyobeba ubainifu juu ya Uislam Iymān na Ihsān.  Na Hakika mwishoni mwa hadithi Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) alisema:

“هذا جبريل أتاكم يعلمكم دينكم”

” Huyu ni Jibriil amekujieni kuwafunza Dini yenu”.
       Na pendekezo hilo limetimia kwa Fadhila za Allāh  kwakuitoa sharh hii katika mwaka huu (1424H).  Na Hakika umekuja kutoka Wanazuoni wengi ubainifu wao juu ya ukubwa wa shani  ya hadithi hii.
Amesema Al-Qādhiy ‘Iyādh (Allāh amraham), kama ilivyo katika sharh ya Imam Nawawiy juu ya sahihi Muslim (1/158):

وهذا الحديث قد اشتمل على شرح جميع وظائف العبادات الظاهرة والباطنة، من عقود الإيمان وأعمال الجوارح وإخلاص السرائر والتحفظ من آفات الآعمال، حتى إن علوم الشريعة كلها راجعة إليه ومتشعبة منه، قال: وعلى هذا نالحديث وأقسامه ألفنا كتابنا الذي سميناه بالمقاصد الحسان فيما يلزم الإنسان؛ إذ لا يشذ شيئ من الواجبات والسنن والرغائب والمحظورات والمكروهات عن أقسامه الثلاثة، والله أعلم

“Na hadithi hii imekusanya sharh ya shughuli zote za kiibada za dhahiri na za siri. Ikiwa ni miongoni mwa itikadi za ki-Iymān na vitendo vya viwiliwili, na ikhlas kwa mambo ya siri na kujilinda kutokana na maafa yanayoingia kwenye matendo.  Mpaka  (husemwa kuwa) elimu zote za ki-sharia  zinarejea kwenye hadithi hii na zimetokea humo.
… Na juu msingi wa hadithi hii na magawanyo yake matatu sisi tumekiandika Kitabu tulichokiita:
 “Al-Maqaasidil-Hisān fiymaa yal-zamul-Insān”
kwani havitoweza kutoka vilivyo   vya wajibu, vya sunnah, vyakujikurubisha (kwa Allāh) pamoja na vya haramu na makruuh havitoweza kutoka katika mganwanyiko mtatu huo, na elimu ipo kwa Allāh
       Na amesema Al-Nawawiy-Allāh amraham- (1/160):
“Na elewa ya kwamba hii hadithi imekusanya aina mbali mbali za elimu na maarifa, adabu na lataaif, bali ndo asili ya Uislam kama tulivyosimulia kutoka kwa Al-Qādhiy ‘Iyādh (Allāh amraham) “.
Na amesema Al-Qurtubiy -Allāh amraham- kama ilivyokuja katika “Al-Fat’h” (1/125):
“Hadithi hii inafaa iitwe Mama wa Sunnah, Kwa kule kusheheni kwake mengi yanayohusu elimu ya sunnah “.
Na amesema Ibn Daqiiq Al-‘Iiid katika “sharhul-Arba’iin”:
“Hii ni sawa na mama katika Sunnah, kama ilivyoitwa suuratil-faaatiha mama wa Qur’an kwa kukusanya kwake maana nzima ya Qur’an”.
Na amesema Ibn Rajab (Al-Hanbaliy) katika “Jaami’ul-Uluumi Wal-Hikam” (1/97):
“Ni hadithi adhimu imekusanya sharh ya Dini nzima. Na ndio maana amesema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) mwishoni mwa hii hadithi:

“هذا جبريل أتاكم يعلمكم دينكم”

“Huyu ni Jibriil amekujieni ili akufunzeni Dini yenu”.
Baada ya daraja la Uislam na Iymān pamoja na Ihsān. Na akayajaalia yote hayo kuwa ndio muunganiko wa Dini”.
Na nimeiita (sharh hii):

شرح حديث جبريل في تعليم الدين

“Sharh ya hadithi ya Jibriil katika kufunza Dini”.
Na namuomba Allāh-‘Azza Wajalla- anufaishe watu kupitia hii (sharh), na awaafiqishe (kwa tawfiiq) wote katika kupata elimu yenye manufaa na kuifanyia kazi.
Hakika yeye ni Mwingi wa usikivu Mwenye kujibu.

 

 

Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadithi Jibriil