33. Shuruti za لا إله إلا الله


{Sharti ya tano}

  1. Kukubali (yale yanayofungamana na shahada) kunakopingana na kuyarudisha (kuyakataa) kuyakubali kwa moyo ulimi na viungo
Na ameshatusimulia Allāh katika Kitabu chake khabari za waliomuamini na wakaikubali لا إله إلا الله kisha Allāh akawaokoa kutokana na adhabu.  Na wale walioikataa Allāh  akawaadhibu.  Kama alivyosema Allāh  Mtukufu:

“وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَاءُوهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَانتَقَمْنَا مِنَ الَّذِينَ أَجْرَمُوا ۖ وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ”

الروم  47

“Na kwa hakika tumetuma kabla yako Mitume kwa jamaa zao. Wakawajia na hoja zilizo wazi (wakazikufuru) nasi tukawaadhibu wale waliokosea na ilikuwa haki (kuwafanya hivyo). Na ni juu yetu kuwanusuru Waumini” Al-Ruum (47).
Na Allāh  amekhabarisha kuhusu watu walioifanyia kiburi لا إله إلا الله na kwamba wanastahiki adhabu kwa sababu ya kiburi chao juu yake. Akasema Allāh Mtukufu:

۞ احْشُرُوا الَّذِينَ ظَلَمُوا وَأَزْوَاجَهُمْ وَمَا كَانُوا يَعْبُدُونَ 22

“Wakusanyeni wale waliodhulumu na washirika wao na vile walivyokuwa wakiviabudia kinyume cha Allāh” (22).
Mpaka katika kauli yake aliposema:

“إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَٰهَ إِلَّا اللَّهُ يَسْتَكْبِرُونَ 35.  وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ “

الصافات 36

“Hakika wao walikuwa wakiambiwa semeni لا إله إلا الله wanafanya kiburi.  Na wanasema: Yawaje kwetu sisi kuwaacha  waungu wetu kwaajili ya mshairi aliye wazimu!?” Al-Sāffāt (35-36).
Na amesema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) katika hadithi ya Abū Muwsā  (Allāh  amridhie):

إن مثل ما بعثني الله به من الهدى والعلم كمث الغيث الكثير أصاب أرضا  فكان منها نقية قبلت الماء فأنبتت الكلأ والعشب الكثير وكانت منها أجادب أمسكت الماء فنفع الله بها الناس فشربوا وسقوا وزرعوا وأصابت منها طائفة أخرى إنما هي قيعان لا تمسك ماء ولا تنبت كلأ فذلك مثل من فقه في دين الله ونفعه ما بعثني الله به فعلم وعلم ومثل من لم يرفع بذلك رأسا ولم يقبل هدى الله الذي أرسلت به

رواه الشيخان

“Hakika mfano wa yale aliyonituma nayo Allāh  katika Uongofu na Elimu ni mfano wa mvua nyingi ambayo imeisibu ardhi.  Kikawepo kipande cha ardhi kizuri (chenye rutuba) kilichoyanywa maji na kikaotesha nyasi na majani mengi.  Na kikapatikana kipande (chengine) kikame ambacho kimeyazuia maji na Allāh  akawanufaisha watu kupitia kipande hicho wakanywa na kunyweshwa (wanyama wao) na wakalima.  Na mvua ikakipata kipande chengine (cha ardhi) ambacho ni tambarare hakizuii maji wala hakioteshi nyasi. Huo ndio mfano wa yule aliyejifunza katika Dini ya Allāh na akanufaishwa kwa yale aliyonituma nayo Allah, akajifunza na akawafunza wenzake, na mfano wa yule ambaye hakujali na hakukubali Uongofu wa Allāh niliokuja nao”.
Ameipokea Bukhari na Muslim.

 

قال مقيده-عفا الله عنه

Katika hadithi hii tukufu Mtume wetu (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) amewagawa watu katika mafungu matatu:
(1).   Wale waliojifunza Dini na wakazifahamu nususi za kisharia kisha wakazifanyia istinbaat na kutoa faida zenye tija  za kielimu.   Na hawa huzifanyia kazi elimu zao na wakatoa wakati wao katika kuwafunza watu na kuwanasihi. Na bila shaka hawa ni bora ya watu.
(2).   Wale waliozihifadhi nususi za Kitabu na Sunnah na wakazifikisha kama walivyozihifadhi lakini hawakuwa ni watu wa Istinbāt pamoja yakuwa wapo katika kheri ila wapo chini ya watu wa kwanza.
(3).   Wale walioipuuzia elimu hawataki kujifunza wala kuifanyia kazi wala kuwanufaisha wengine.  Na hawa ndio sharrul-Bariyyah.

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah