34. Shuruti za لا إله إلا الله


{Sharti ya sita}

  1. Kunyenyekea (kwa yale yaliyolengeshwa na لا إله إلا الله ) kunakopingana na kuacha.
Kama alivyosema Allāh  Mtukufu:

وَأَنِيبُوا إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَأَسْلِمُوا لَهُ   الزمر ٥٤

“Na elekeeni kwa Mola wenu na mnyenyekee kwake (kwa utii)” Al-Zumar (54).
Na amesema Allāh Mtukufu:

۞ وَمَن يُسْلِمْ وَجْهَهُ إِلَى اللَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ ۗ   لقمان ٢٢

“Na yeyote atakayeitika kwa Allāh  (kunyenyekea na kutii) ilhali ni Muhsin (yaani Mtu wa Tawhiid) kwa hakika atakuwa ameshika kishiko madhubuti” Luqman (22).
Ama yule ambaye hatousalimisha uso wake kwa Allāh na wala hakuwa ni mtu  wa Tawhiid bila shaka hatashika kishiko kilicho madhubuti.  Kama alivyosema Allāh Mtukufu:

“وَمَن كَفَرَ فَلَا يَحْزُنكَ كُفْرُهُ ۚ إِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ فَنُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا ۚ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ 23 نُمَتِّعُهُمْ قَلِيلًا ثُمَّ نَضْطَرُّهُمْ إِلَىٰ عَذَابٍ غَلِيظٍ”

لقمان 24

“Na yeyote atakayekufur basi usikuhuzunishe ukafiri wake (na kukupa simanzi) kwani ni kwetu ndiko kwenye marejeo yao, tutawapasha khabari kwa yote waliyotafanya.  hakika Allāh  ni Mwingi wa kuyajua yaliyo vifuani. Tutawastarehesha  kidogo (hapa duniani) kisha tutawasweka kunako adhabu kali (akhera)” Luqman (23-24).
Na amesema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam):

“لا يؤمن أحدكم حتى يكون هواه تبعا لما جئت به”

قال النووي: روينا في كتاب الحجة بإسناد صحيح

“Hatoamini mmoja wenu mpaka pale matashi yake yaendane na niliyokuja nayo”.
Amesema Imam Nawawiy:  Tumeipokea kutoka katika kitabu “Al-Hujjah” kwa Isnadi ambayo ni sahihi.

قال مقيده-عفا الله عنه

Hii hadithi wameisahihisah baadhi ya Wanazuoni na wengine wameidhoofisha, na kwenye udhaifu ina ukaribu zaidi kuliko kwenye usahihi.
Imedhofishwa na Al-Imam Al-Albāniy (Allāh amraham), na amesema Ibn Baaz (Allāh amraham):

“والحديث في إسناده ضعف لكن معناه صحيح”

“Na hadithi katika Isnadi yake kuna udhaifu lakini maana yake ni sahihi”.

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah