35. Shuruti za لا إله إلا الله


{Sharti ya saba}

  1. Kuipenda (لا إله إلا الله ) na yote yatokanayo na kalimah hiyo. Na kuwapenda watendaji wa hiyo kalimah. Na kuvichukia vinavyokwenda kinyume na hiyo kalimah
Na maana ya hayo ni kuwa na msingi wa Al-Walaa (yaani mapenzi kwa watu wake) na Al-Baraa (kujiweka mbali na wasiokuwa watu wake).  Kama alivyosema Allāh  Mtukufu:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا آبَاءَكُمْ وَإِخْوَانَكُمْ أَوْلِيَاءَ إِنِ اسْتَحَبُّوا الْكُفْرَ عَلَى الْإِيمَانِ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُون

 التوبةَ 23

“Enyi wale mlioamini! Msiwafanye  baba zenu na ndugu zenu kuwa ni marafiki vipenzi pale wanapokhitari ukafiri  dhidi ya Iymān, na yeyote atakayewafanya ni marafiki (vipenzi) basi hao ndio madhalimu” Al-Tawbah (23).
Na amesema Allāh  Mtukufu:

“وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ     ” المائدة ٥١

“Na yeyote atakayewafanya ni marafiki basi naye ni katika wao” Al-Māidah (51).
Na amesema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) katika hadithi ya Abū Hurayrah (Allāh amridhie):

“لا يؤمن أحدكم حتى أكون أحب إليه من والده وولده والناس أجمعين”

رواه الشيخان

“Hawezi akawa ni mu’mini mkamilifu wa Iymān mmoja wenu mpaka niwe napendeza zaidi kwake kuliko mzazi wake, watoto wake na watu wote kwa ujumla”.
Ameipokea Bukhari na Muslim.
Na amesema Allāh Mtukufu katika kushurutisha kumfata (kikamilifu) Mtume wake (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam):

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ 31 قُلْ أَطِيعُوا اللَّهَ وَالرَّسُولَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ

آل عمران32

“Sema: Kama kweli mnampenda Allāh  basi nifuateni mimi  atakupendeni Allāh  na atakusameheni madhambi yenu na Allāh  ni Mwingi wa msamaha Mwingi wa rehema.  Sema: Mtiini Allāh  na Mtume na kama mtakengeuka basi kwa hakika Allāh  hawapendi makafiri” Al-Emran (31-32).

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah