37. Mafunzo tuyapatayo katika Shuruti za لا إله إلا الله


(2).   Ni wajibu kumpenda Allāh na Mtume wake (na hiyo ni sharti miongoni mwa Shuruti za لا إله إلا الله), pia ni wajibu kuwapenda Waumini na kuwachukia makafiri na kuwafanya kuwa ni maadui.  Na kwa hakika Amesema Allāh  Mtukufu:

“إِنَّ الْكَافِرِينَ كَانُوا لَكُمْ عَدُوًّا مُّبِينًا    ” النساء 101

“Hakika makafiri kwenu ni maadui waliowazi” Al-Nisāi (101).
Na ni wajibu uadui kwa makafiri uwe wazi wa milele, Ila kama itachelewa (jambo) kutoka kwao hautodhihirishwa. Amesema Allāh:

إِلَّا أَن تَتَّقُوا مِنْهُمْ تُقَاةً ۗ     ” آل عمران ٢٨

“Ila (ikiwa mnafanya urafiki nao wa juu juu tu hivi) kwa ajili ya kujilinda na shari zao. Al-‘Imrān (28).

Na kwa hakika amesema Allāh  kuhusu Ibrāhiim (‘Alayhis-Salaam) na wale walio pamoja naye:

“إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآءُ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّهِ وَحْدَهُ”

الممتحنة ٤

“Waliposema  kuwaambia watu wao: hakika sisi tupo mbali nanyi, na vile vyote mnavyoviabudia kinyume cha Allāh, tumewakana, na umeshadhihiri baina yetu na baina yenu uadui na bughdha ya milele mpaka mumuamini Allāh  peke yake” Al-Mumtahanah (4).

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim:  http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah