40. Masāili muhimu yanayofungamana na kuihakikisha لا إله إلا الله


(a).   Yeyote atakayeshahadia kuwa hakuna mola anayepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allāh, na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allāh, basi ni wajibu juu yake kuisimamia kwa haki yake (shahada hiyo), kama vile kutekeleza faradhi na kuachana na yale aliyoyaharamisha Allāh  juu yake.
Na yeyote atakayetamka shahada mbili hatopinga kutekelezwa juu yake adhabu hapa duniani (kwa kosa alilotenda) eti kwakuwa ametamka shahada mbili.  Hivyo kama akitamka shahada mbili lakini akagoma kutoa zaka -mathalan- hakika atapigwa vita juu ya hilo kwa sababu (hilo) ni miongoni mwa haki za shahada mbili.
Kama alivyosema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam):

“أمرت أن أقاتل الناس حتى يشهدوا أن لا إله إلا الله وأن محمدا رسول الله ويقيموا الصلاة ويؤتوا الزكاة”

رواه الشيخان

“Nimeamrishwa nipambane na watu mpaka washahadie kuwa لا إله إلا الله na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allāh, na wasimamishe swala na watoe zaka”.
Ameipokea Bukhari na Muslim.
Na hakika Abūbakr alipambana na waliogoma kutoa zaka. Kwa sababu kutoa zaka ni haki ya mali.
Na kupambana kwake na waliogoma kutoa zaka ni kwa ushahidi wa maneno ya Mtume wa Allāh (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam):

“فإذا فعلوا ذلك عصموا مني دمائهم وأموالهم إلا بحقها وحسابهم على الله”

“Wakilikubali hilo (la kushahadia) basi watazikinga kutokana nami damu zao na mali zao isipokuwa kwa haki yake (shahada hiyo), na hesabu yao ipo kwa Allāh”.
Ameipokea Bukhari na Muslim.

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah