08.Faida katika Hadeeth ya Jibriyl-03


Katika kisa alichokileta Imam Muslim kabla ya mlolongo wa hadithi (yenyewe), kutoka kwa Yahya bin Ya’mur na Humayd bin ‘Abdirrahman Al-Himyariy kuna faida nyingi:
(1). Ni kwamba bida’ah ya kukanusha Qadar ilidhihiri Basrah (Iraq) katika kipindi cha uwepo wa Maswahaba na uhai wa Ibn ‘Umar. Ambaye kifo chake kilikuwa mwaka 73H.
(2). Kurejea kwa Matābiina kwa Maswahaba (wa Mtume swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) katika kujifunza hukumu ya mambo yanayotatanisha, sawa sawa iwe yanahusu itikadi au mengineyo. Na hili ndilo jambo la wajibu juu ya kila Muislam arudi katika kutaka ufumbuzi wa mambo yake kwa Wanazuoni. Kwa ushahidi wa maneno ya Allāh-‘Azza Wajalla-:

فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ     ” النحل 43

“Waulizeni Wanazuoni ikiwa hamjui” Al-Nahl (43).

 

 

Muhusika: Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbād Al-Badr
Mtarjim:http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Sharh Hadithi Jibriil